Mashindano ya Tenisi ya meza ya ulimwengu yanaahirishwa tena kwa sababu ya virusi ya Corona

Mashindano ya Tenisi ya meza ya ulimwengu,  yaliyopangwa kufanyikwa katika mji wa  Busan huko Korea Kusini  yaliahirishwa tena mnamo Jumanne kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona.

Korea Kusini ilikuwa moja ya nchi za kwanza kushambuliwa na virusi ya "Covid-19" nje ya Uchina, kitovu cha kwanza cha janga hili, na ilikuwa nchi ya pili kwa suala la idadi ya maambukizi ulimwenguni kabla ya kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Mnamo mwezi wa Februari, kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya maambukizi kuliwahimiza maafisa kuahirisha mashindano ya Tenisi ya meza ya ulimwengu yaliyopangwa kati ya Machi 22 na 29, hadi mwishoni mwa Juni.

Pamoja na mlipuko wa "Covid-19" kote ulimwenguni, ambapo zaidi ya watu 73,000 waliuwawa kati ya kesi za maambukizi milioni  1.32 zilizothibitishwa hadi sasa, uamuzi wa kihistoria ulifanywa wa kuahirisha Michezo ya Olimpiki kutoka majira ya joto ya 2020 hadi majira ya joto ya 2021.


Shughuli zote za Shirikisho la Kimataifa kwa Tenisi ya meza zilisitishwa hadi mwisho wa Juni, basi uamuzi huo ulirekebishwa Jumanne kuhusu mashindano ya ulimwengu ya timu, ambapo Miadi mpya ya muda imewekwa kati ya Septemba 27 na Oktoba 4.



Shirikisho la Kimataifa la mchezo huo lilionyesha katika taarifa yake kwamba kamati iandaayo ya kitaifa itaendelea kufuatilia hali hiyo "kwa kipaumbele cha kupewa afya na usalama wa wachezaji, makocha, mashabiki na maafisa."


Virusi vya Corona vilisababisha machafuko makubwa katika matukio ya michezo ulimwenguni kote, na vilisababisha kuahirishwa matukio mengi hata kufanya uamuzi wa kufuta baadhi yao.

Comments