Kuahirisha Ligi ya Mabingwa wa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa muda usiojulikana
- 2020-04-12 15:34:03
Shirikisho la Afrika la Soka “CAF” lilitangaza kuahirisha mechi za nusu ya fainali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, kwa muda usiojulikana.
timu za Al-Ahly na Al-Zamalik zilifikia dura ya nusu ya fainali ya Ligi ya Mabingwa na timu ya pyramids ilifikia dura ya fainali ya Kombe la Shirikisho.
Shikisho la kiafrika lilisema katika taarifa iliyotangazwa kupitia mtandao rasmi yake kwamba “ kwa kuzingatia wasiwasi unaokua na mabadiliko ya COVID-19 na kukiwa na mashaka na kupiga marufuku katika nchi nyingi, tume ya dharura ya CAF ilichukua hatua ya kuahirisha mechi zinazofuata kwa muda usiojulikana:
- Mechi za nusu ya fainali za Total CAF , Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho CAF
mechi za kwenda na kurudi zilizopangwa kutoka 1-3 Mei na 8-10 Mei 2020
- Fainali za FIFA , Kombe la Ulimwengu chini ya umri wa 17 kwa wanawake: zilizopangwa kutoka 1-3 Mei na kutoka 15-17 Mei 2020
Na ratiba mpya itatangazwa mnamo wakati unaofaa.
Wakati huo huo, CAF inafuatilia hali hiyo kwa karibu na inafanya kazi na wadau kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya athari ya virusi kwenye bara hilo.
Comments