Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikubali kuzindua Redio ya Vijana wa Misri kwenye mitandao, ili iwe jukwaa jipya la vyombo vya habari linaloshikilia kasi na nyakati na linachangia mawasiliano pamoja na vijana wa Misri wa vizazi vyote.
Waziri wa Vijana alisisitiza kuwa Redio ni chanzo kipya ndani ya mfumo wa vyombo vya habari kwa Wizara ya Vijana, ambayo iliitwa lango la Misri kwa Vijana na Michezo , ambapo hadi sasa linajumuisha tovuti rasmi ya Wizara na idhaa ya YouTube iliyozinduliwa mwezi uliopita pamoja na njia kadhaa za mawasiliano ya kijamii, Twitter na Instagram.
Programu zitatangazwa katika nyanja zote zinazohusiana na vijana na michezo, na taarifa ya moja kwa moja kwa shughuli zote za Wizara katika machapisho yak e tofauti, idara, vituo vya vijana na miji.
Waziri wa Vijana aliongezea kuwa utangazaji wa majaribio ya redio ulianza leo Ijumaa na kuanza kwa siku ya kwanza ya Ramadhani, kutayarishwa na kutangaza programu 23 kila siku na kila wiki, kama kikundi cha kazi, ambacho ni vijana wenye talanta, kiliandaa na kuwasilisha vipindi hivi chini ya usimamizi wa mhariri wa lango la Misri kwa Vijana na Michezo Bwana Gamal Nour El Din kwa kushirikiana na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Vyombo vya habari Bwana Mohamed El Shazly.
Pamoja na kufaidika kutoka kwa utaalam na alama za redio ya kimisri, kama , Mheshimiwa Fahmy Omar, Kamel Al-Bitar, Omar Battaysh, Ashraf Mahmoud, na wengine wanaojulikana.
Waziri wa Vijana alisisitiza kwamba kuna mishangao mengi kwa wasikilizaji wa redio ambayo itatangazwa wakati wa siku zijazo, na pia tumezingatia kwamba kuongezeka kwa mipango ya burudani na mashindano na tuzo wakati wa mwezi wa Ramadhani kwa vijana wasikilizaji , na mipango iliyotangazwa kuanzia leo ni kama :
Vipindi vya Redio ya Vijana wa Misri:
1- Afrika kwenye mitandao
2 - Siri za pesa
3- ukiwa msahau
4- Mwanangu ni nguzo
5- Dini na dunia yako
6- Viti viwili na meza
7- kauli muhimu
8- Mpira kwenye mitandao
9- amekuambia wapi?
10 - Anayeamsha watu kwa Daku kwenye mitandao
11 - Mhusika na taarifa
12- Hadithi ya methali
13- Sura na Ibtihali
14 - Koti nyeupe
15- Mimi na Mamangu
16-Mpira wa soksi
17 - idumu Misri
18- Alvar hakam El Meshwar
19- Ramadani Kareem ewe Mpira
20 - Nahlan wa Sahlan
21-Vijana wetu ni wazuri zaidi
22-Tuzo kwa Nani?
23- Kwenye mlango wa Wizara
24-Logharitmiki
Comments