Waziri wa Vijana na Michezo afungua majengo kadhaa vya kimichezo ndani ya klabu ya El Oboor
- 2020-04-26 22:38:30
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Meja Jenerali Abd El Hamid El Hagan, Gavana wa Qalyubia, pamoja na Mshauri Hossam Abd El Aziz, Mwenyekiti mkuu wa Klabu ya El Oboor, kufungua vituo kadhaa vya kimichezo ndani ya klabu ya El Oboor.
Ufunguzi huo ni pamoja na uwanja wa kisheria kwa klabu, unaokuja ndani ya mpango wa Wizara ya Vijana na Michezo kuboresha viwanja kwenye klabu, ambapo uzio mmoja umetengenezwa kuzunguka uwanja huo, umeangaziwa kwa mfumo wa taa za kisasa, nyasi za viwandani katika uwanja, na pia maktaba ya klabu kwa lengo la kuwahudumia wanachama, na kufungua ukumbi wa Uzima wa mwili na shughuli za kutumia ardhi.
Wakati wa tembezi hilo, Waziri wa Vijana na Michezo alisikiliza maelezo ya kina kutoka kwa maafisa wa klabu juu ya shughuli muhimu zaidi zilizokuwa zikitekelezwa kabla ya kusimamisha shughuli ya kisasa ya michezo, kupambana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona, na kiwango cha matumizi bora ya vijana kutoka kwake, na alikubali utafiti uliopendekezwa kwa bodi ya idara ya klabu kwa kuanzisha hoteli ya kuhudumia wachezaji na timu za kimichezo ndani ya klabu.
Waziri wa Vijana na Michezo alisema kuwa msaada wa serikali kwa shughuli za kimichezo haujawahi kufanywa hapo awali , na kuna juhudi za kukuza majengo ya kimichezo na kupanua nafasi ya ushindani miongoni mwa vijana na kuwahimiza wafanye shughuli za kimichezo ili kujiendeleza kimwili, kiakili na kisaikolojia, na kunufaika na nguvu zao kutokana na mazoezi ya michezo ili kujenga kizazi cha vijana ambao wakijengwa vizuri na wenye maadili.
Waziri wa Vijana na Michezo aliashiria kuwa kuna mawasiliano na uratibu pamoja na mkoa wa Qalyubia katika kutoa msaada na kukuza maendeleo ya vituo kadhaa vya kimichezo na shime ya nchi katika kukuza sekta ya vijana na michezo na kuwasaidia vijana na kutumia uwezo wao vizuri.
Sobhy ameongeza kuwa kuna miradi ya maendeleo ambayo ni pamoja na klabu na vituo vya vijana katika mikoa tofauti, ndani ya mpango wa uwekezaji wa Wizara.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Abd El Hamid Al-Hajan, Gavana wa Qalyubia, alimkaribisha Waziri wa Vijana na Michezo kwenye ardhi ya mkoa huo, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kamili pamoja na Wizara ya Vijana na Michezo ili kuendeleza sekta ya michezo na kukuza majendo ya vijana ili kupanua nafasi ya mashindano ya michezo.
Wakati wa mkutano wake na Waziri wa Vijana na Michezo, Gavana wa Qaliubiya alionyesha juhudi za Wizara za kuendeleza sekta ya michezo na kuendeleza vituo vya vijana na shughuli zinazofanywa kwa Kurugenzi la Vijana na Michezo kuwasaidia vijana na kufaidika kutoka nguvu zao kupitia mazoezi.
Comments