Japan yadokeza uwezekano wa kufutwa Olimpiki ya Tokyo ikiwa itaahirishwa baada ya 2021

 Jumanne, Gazeti la Japan lilinukuu kauli ya Yoshiro Mori rais wa Olimpiki ya Tokyo 2020, kwamba Japan itafutwa kukaribisha  michezo hiyo ikiwa haiwezi kufanyika mnamo 2021 baada ya kuahirishwa  kwa mwaka mmoja.

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa ilikubaliana na serikali ya Japan mwezi uliopita kuahirisha Olimpiki hadi Julai 2021 kutokana na janga la virusi ya Corona, ambalo liliwaua maelfu ulimwenguni kote.

Lakini pamoja na kuongezeka idadi ya watu walioambukizwa na vifo kote ulimwenguni, na wataalam wanaotarajia kuwa itachukua muda mrefu kabla ya kutoa chanjo ya virusi vipya, maswali yameongezeka kuhusu uwezekano wa kuahirisha zaidi.


Na Kujibu swali la uwezekano wa kukaribisha Tokyo kwa Olimpiki ikiwa iliahirishwa hadi 2022, "Morey" alisema katika mahojiano na gazeti la Nikan la michezo la kijapan "Hapana, kwa kesi hii Olimpiki itafutwa."


Lakini waziri mkuu wa zamani bado anahisia tumaini kuhusu uwezekano wa kufanyika Olimpiki mnamo 2021.


Na gazeti lilinukuu kutoka Morey akisema"Tumeamua kuahirisha Olimpiki hadi majira ya joto yajayo, baada ya kushinda vita.


Aliongeza, "Olimpiki itakuwa ya thamani zaidi kuliko michezo yoyote iliyopita ikiwa tutafanikiwa kuifanyika baada ya kushinda vita hii. Lazima tuamini jambo hilo, au hatutapata mavuno ya bidii yetu kubwa . "


Masa Takaya msemaji wa Olimpiki ya Tokyo 2020, aliulizwa kuhusu maoni ya "Morey", lakini alisisitiza kwamba uangalifu wa waandaaji upo kwa mwaka ujao.


Takaya alisema katika taarifa ya waandishi wa habari

"Tarehe mpya za michezo ya Tokyo 2020 zimewekwa tayari, na dhamira yetu ni kukaribisha michezo hiyo mwaka ujao.



na aliongeza kuwa "Morey": "Alitoa maoni haya kwa kuzingatia maoni yake."


Wakati wa mkutano wa waandishi wa habari, Morey alipendekeza kushiriki michezo ya Olimpiki na Olimpiki kwa watu wenye mahitaji maalum kwa sherehe za ufunguzi na kufunga badala ya muundo wa kawaida kwa kufanyika sherehe mbili kwa michezo yote.


"Morey" alisema kuwa jambo hili litapunguza gharama licha ya wazo linabaki gumu baada ya Tokyo tayari kuuza tiketi za sherehe nne.


Takaya alisisitiza kwamba suala hili limezungumziwa lakini bado hakuna mipango kamili.


na aliongeza " Kwa sababu ya athari ya virusi ya Corona, hali itakuwa tofauti kabisa mwaka ujao," . Masuala mengine muhimu, pamoja na sherehe, lazima kuzingatiwa tena "


Kamati iandaayo ya Olimpiki na Kamati ya Olimpiki ya kimataifa bado zinajadili gharama za kuahirisha Michezo.


Bajeti ya Olimpiki ilifikia bilioni Dola 12.6 kabla ya kuahirishwa, wakati vyombo vya habari vya Japan vilisema kwamba kufanyika Michezo mnamo 2021 inaweza kusababisha gharama kuongezeka kwa bilioni yen 300 (bilioni Dola2.8 ).


Takaya alisema kuwa mchakato wa kuangalia kwa gharama unaendelea, lakini alikataa tangazo la kamati iandaayo  "idadi kubwa ya bilioni yen 300."


Zaidi ya watu milioni tatu wameambukizwa, wakati zaidi ya watu 210,000 ulimwenguni wamekufa kutokana na virusi vya Corona.

Comments