Ahmed Ahmed, Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), alitoa maoni yake kwa hakika ya kugombea kwake katika uchaguzi ujao wa CAF uliopangwa kufanyika 2021.
Na kupitia akaunti yake rasmi kwenye tovuti ya mitandao ya kijamii «Twitter»: Ahmed alisambaza "Tangu asubuhi ya leo, nasoma makala za waandishi wa habari zinazoelezea kugombea kwangu kwa muhula nyingine kama Rais wa Shirikisho la Afrika .
Aliongeza, "nazingatia tu katika kukabiliana na mgogoro la janga la Corona, na nitakapochukua uamuzi ,mimi ndimi nitautangaza "
Ahmed Ahmed ameshika urais wa CAF tangu 2017 baada ya kushinda uchaguzi mbele ya Essa Hayatou wa Kameron.Na taarifa kadhaa zilisambaza nia ya Mhandisi Hani Abu Rida, Rais wa zamani wa Shirikisho la Misri, na mjumbe wa Ofisi ya Utendaji kwenye mashirikisho mawili ya Soka ya Kimataifa na Afrika, kuingia uchaguzi wa Shirikisho la Afrika.
Comments