Muhamed Fadl anadhihirisha mishangao ya safari ya Hirizi ya mataifa ya Afrika 2019.

Muhamed Fadl "Mkurugenzi wa michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika "alionyesha maelezo ya safari ya kazi iliyoendelea kwa miezi kadhaa ili kutoa Hirizi inayofaa kwa michuano inayokaribishwa nchini Misri 2019.

 

Fadl alisema kwamba wakati mdogo ulikuwa chngamoto kubwa mbele ya Misri katika masuala yote ya michuano na Hirizi ile haikuwa msamaha kwa hayo.

 

Alieleza akisema: tulifanya kazi kwa utaratibu kati ya suala la maendeleo ya uwanja, kuandaa uwanja wa mafunzo, Hoteli, kuchagua wanaojitolea, sherehe ya kutoa kura, masuala ya kutangaza, uangalifu, tiketi za mechi na kuzitangaza, na mipango ya kiusalama ya kuzihudhuria, na inayohusiana na michuano mikubwa zaidi katika historia ya bara la Afrika kwa ushirikiano wa timu 24 kwake.

 

(Kampuni ya kimisri)

Alieleza pia "Hirizi" ilifanyika kwa kampuni ya kimisri ambayo haikupata pesa yoyote kwa jambo muhimu  hilo, na hii ili kutoa huduma nzuri kwa Misri na kampuni hii ni (Aroma).

 

Aliendelea kampuni ilifanya bidii ili kutoa Hirizi katika wakati mdogo na kwa ufanisi unaohitajika kusifwa na kuthaminiwa toka tume iandaayo.

 

Aliongeza "baada ya hiyo tulielekea Uingereza kwa ajili ya kutoa Hirizi katika kampuni iliyounda Hirizi ya Kombe la dunia 2018, na michuano ijayo ya mataifa ya ulaya.

 

Alisisitiza kwamba "Utoaji wa Hirizi kwa njia nzuri zaidi  ulikuwa kazi ya kwanza ya tume iandaayo ili kusaidiana kutoa picha nzuri, changamfu na sherehe kwa Misri katika michuano. "

 

(TOT)

Fadl alizungumzia shujaa wa Hirizi, mhusika wa TOT uliochaguliwa ili uwe Hirizi ya michuano.

 

Alieleza"TOT ni mtoto mmisri anapenda mpira wa miguu, tulichora mhusika wake kutoka kitambulisho  cha kimisri ili anatufanana sana, na kukieleza na kukiwakilisha kizazi kipya ili kutupa Amali kwa Mustakbali.

 

Aliendelea "tulichagua awe shujaa mwenye umri mdogo ili kuwakilisha vizazi vipya na Mustakbali yake.

 

Alisisitiza kwamba" miongoni mwa malengo ya tume iandaayo ni kuchora mustakbali nzuri, kutoa makada wapya, na kutoa masuala muhimu kwa kampuni za kimisri na kuboresha miundombinu ya uwanja utakayotufaidisha kwa miaka mirefu".

 

(Kazi inaendelea)

 

Aliongeza"  Pamoja na kampuni ya (Senregy) tunafanya kazi ya kutoa wimbo rasmi kwa michuano kwa lugha tatu nazo ni (Kiarabu, Kiingereza, na Kifaransa) ".

 

Alitimiza kauli yake "sasa kazi inaendelea kwa kutekleza faili za michuano zinazobaki, bado tuna kazi nyingi na wakati mdogo lakini tuna imani kubwa ya mafanikio. ""

Comments