Wizara ya Vijana na Michezo ya kimisri yazindua Mpango wa viongozi wa Vijana kutetea bara la Afrika katika kupambana na migogoro na shida

Chini ya uangalizi wa Profesa Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Wizara ya Vijana na Michezo ilizindua mpango wa viongozi wa Vijana kutetea bara la Afrika katika kupambana na migogoro na dhiki, hasa athari hasi zinazotokana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona COVID 19 chini ya anwani ya "Walinzi wa Afrika"


Tukiamini kwamba vijana ndio ngao ya usalama na kinga kwa nchi zao na njia ya kwanza ya ulinzi kwa misiba inayolikabili bara hilo, na  bara la Afrika ni sehemu moja na chombo kilichounganika,  mnamo vipindi vilivyopita tumehangaika kuandaa vijana wake na kuwawezesha kuongoza, na wakati wa kisasa ndio unaofaa kabisa kupata tija kutoka hayo yote na kuhakikisha kuwa vijana hawa ni madhubuti na wenye ushawishi , wana jukumu chanya na wana uwezo wa kushiriki na kusaidia katika  kupunguza athari hasi zinazotokana na mgogoro huo, hata mpango huo uwe kituo ambacho kinawasiliana na viongozi wa vijana wanaofanya katika sehemu zote za bara hili ili kuangazia mwanga kwao , kuonyesha jukumu lao na kuwatambulisha kama mfano kwa vijana wote wa bara.

Comments