Chumba maalumu cha kujitayarisha kwa timu kwenye uwanja wa michezo wa Kairo.

Bwana Muhamed Fadl " Mkurugenzi wa tume inayoandaa kombe La mataifa ya kiafrika" alitembea uwanja wa Kairo ili kuangalia maendeleo ya majengo ya uwanja unaopokeza mechi za timu ya Misri, ufunguzi, na mwisho wa michuano.

                                            

Na mnamo  siku ya Alhamisi bwana Fadl alisisitiza kutembea pembe zote za uwanja ili kuangalia yote yanayohusu mahali pa kuingia mashabiki, huduma za kiafya zinazopatikana kuzunguka Daraja au kuzunguka kwa uwanja.

 

Fadl amesema kwamba shughuli zote zinafanyikwa kwa uhodari,  akieleza:"tunafuatia kazi ya kuboresha uwanja mpaka uwe katika sura adhimu".

 

Fadl amesisitiza kwamba : kazi ya maendeleo inaendelea vizuri kwa yote, kwa mfano:  kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Kairo tuliamua kuunda chumba maalumu cha ndani cha kujitayarisha kwa timu kulingana na nyanja nyingi za kimataifa. 

 

Amekwisha kauli yake :" lengo letu ni kuacha nguzo nzuri ya kimichezo kwa mpira wa kimisri, itakayotuheshima katika kombe la mataifa ya kiafrika na kuitumia baadaye kwa miaka".

Na michuano hutolewa katika tarehe ya 21,mwezi wa Juni kwa kushirikiana na timu 24 kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la mataifa ya kiafrika, na itaendelea kwa tarehe ya 19, mwezi wa Julai.

Comments