Hivi karibuni, tangazo la programu ya kwanza ya vijana kwa Kiingereza inayoitwa "Global Citizen Talks"

Wizara ya Vijana na Michezo, inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, "Ofisi ya Vijana wa Kiafrika na Idara kuu kwa Programu za Kiutamaduni na za Hiari", yazindua "Programu ya Raia wa kimataifa" " Global Citizen" , inayotangazwa kwa Kiingereza moja kwa moja kwenye majukwaa tofauti ya vyombo vya habari vya kijamii (kurasa za facebook, Instagram, Twitter, youtube, LinkedIn ), inayopokea watoa maamuzi na wenye Hadhi za kimataifa katika nyanja nyingi tofauti ulimwenguni na kutoka Misri.

Programu hiyo inalenga kuunga mkono dhana ya Umoja na ushirikiano wa ulimwengu, kuelekeza ujumbe chanya kwa vijana wa ulimwengu kutoka Kairo, kuonyesha uzoefu wa mafanikio wa vijana kote ulimwenguni, kupanua upande wa kiutamaduni kati ya vijana kwa kuingiliana pamoja na kupanua madaraja ya mawasiliano kati ya vijana kupitia mawasiliano halisi na ujihusishaji wa moja kwa moja na vijana wenye usuli tofauti. Na kuandaa viongozi wa vijana wanaoweza kufanya mabadiliko ya kweli.

Hii inatoka kutoka kwa imani ya Wizara ya Vijana kwa umuhimu wa jukumu la vijana katika kupambana na misiba ya ulimwengu na wawe katika mistari ya mbele inayolenga kueneza ufahamu wa hatari za magonjwa na njia za kujikinga na kubuni mipango inayokidhi mahitaji tofauti, sawa yakiwa ya kiafya, kiuchumi, kijamii au kisiasa.

Comments