Katibu mkuu wa shirikisho la soka la Kiafrika (CAF), Abd Almoneem Bah, ametangaza miadi ya michuano ya kombe la mataifa ya Kiafrika iliyopangwa kufanyika nchini Cameron.
Bah, wakati wa taarifa za waandishi wa habari, alisema kwamba michuano ya mataifa ya Kiafrika itafanyika katika miadi yake iliyopangwa hapo awali, mnamo mwezi wa Januari, mwaka ujao.
Na kuhusu kuendelea kwa mashindano ya mabara mengine, alisisitiza kwamba " bado kuna awamu nne katika fainali za mataifa ya Kiafrika 2021, na tunaweza kucheza mechi mbili mnamo kila mwezi, jambo ambalo linahitaji miezi minne ambayo ni Juni ,Septemba, Oktoba na Novemba, mnamo mwaka huu".
Pia Bah alisema : michuano ya mataifa ya Kiafrika itafanyika katika miadi yake iliyopangwa mnamo miezi miwili Januari na Februari, na maneno yoyote juu ya kuahirisha si kweli, na sababu ya kipekee inayotufanya kuchukua maamuzi ya kuahirisha ni kuendelea kwa kuenea virusi vya Corona mpaka mwisho wa mwaka huu barani Afrika.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka la Kiafrika aliongeza kusema : mpaka sasa, tunayo mtazamo kwa kufanyika michuano ya Kiafrika katika miadi yake, na tunasubiri kumaliza kwa virusi vya Corona mnamo kipindi kijacho na mwisho wa hatua za tahadhari.
Na kuhusu kufanyika michuano ya (CAN) mnamo majira ya joto alisema : haiwezekani kufanyika michuano mnamo majira ya joto kwa sababu ya hali za hewa nchini Cameron mnamo miezi, Juni na Julai 2021, jambo lililotufanya kuchukua maamuzi tangu muda kwa kufanyika michuano mnamo majira ya baridi nchini Cameron, mnamo mwaka ujao, kabla ya kuonekana kwa virusi vya Corona.
Comments