Mkutano wa tatu wa kimataifa kwa utamaduni wa michezo wajadili marekebisho ya mwenendo wa michezo

  shirikisho la Misri la utamaduni wa michezo, kwa kushirikiana  na mashirika ya Kiarabu na Kiafrika, chini ya ulinzi wa Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Mkuu wa Ofisi ya kiutendaji wa Baraza la Mawaziri la Vijana na Michezo, na msaada kwa Idara ya Michezo katika Ligi ya Nchi za Kiarabu, Shirikisho la Kamati za Olimpiki za Kiarabu na Shirikisho la Konfedralia ya kimichezo ya kiafrika, zinaunda Mkutano wa tatu wa kisayansi juu ya utamaduni wa michezo chini ya kichwa.  " marekebisho ya mwenendo kwa ajili ya michezo yenye Usalama zaidi ulimwenguni."


 Mkutano huo katika vikao 6 kwa muda wa siku mbili , unajadili kila kitu kinachohusiana na kurudi salama kwenye michezo, na inayohitajika kurekebisha mwenendo katika taratibu, sheria, haki za udhamini au mikataba.


 Kwa upande wake, Mwandishi wa Vyombo vya habari Ashraf Mahmoud , Rais wa Mshirikisho ya Kimisri, Kiarabu na Kiafrika ya Utamaduni wa Michezo na Rais wa Mkutano huo, alisema kuwa kuanza kwa mkutano huo itakuwa saa sita mchana Jumanne, siku ya pili kutoka Juni ijayo, na kikao cha ufunguzi wa sera salama na taratibu za kurudi kwa michezo, ambayo mdhamini wa mkutano huo, Dokta Ashraf Sobhy na Sheikh Saud Al Abd Al Aziz "Katibu mkuu wa Shirikisho la tume za kiolimpiki za kitaifa za kiarabu", Waziri mwakilishi Abd ElMonim Al Shairi"Mkurugenzi wa idara ya Michezo huko jumuiya ya nchi za kiarabu" watazungumza, na kikao cha kwanza kitakuwa na kichwa cha kurekebisha mwenendo na kuweka masharti ya michezo yenye Usalama zaidi.


 Dokta Abouna Paul, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani, Profesa Michele Kuluchi, mjumbe wa Baraza la Maazimio ya Shida la FIFA, Mogan Kreikbe, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Utamaduni wa Michezo, Dokta Muhamad Sultan, Mwenyekiti wa Kamati ya Matibabu ya Wizara ya Vijana na Michezo, na Dokta Sabaa Jarrar, Rais wa Shirikisho la Palestina kwa Utamaduni wa Michezo, wote wanazungumza.


 Kikao cha pili kitaangazia athari ya tuzo hiyo juu ya sheria za michezo fulani.Akizungumza na Meja Jenerali Ahmed Nasser, Rais wa Shirikisho la Afrika, na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya Kiarabu, Dokta Raja Allah Al-Salami, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Waarabu, na Ayed Mabkhout, Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Emirates Al-Jazira na Bingwa wa Olimpiki wa Morocco Nozha Badwan, na Lotfy Laabid Rais wa Shirikisho la Tunisia la Triathlon.


 Kikao cha tatu kitajadili: mkakati wa kudumisha ukuaji kwa tasnia ya michezo, ambayo Dokta Imad Al-Bennani, Rais wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa na Rais wa Mashirikisho ya  kimisri, Kiarabu na kiafrika kwa Michezo kwa Wote, pia Profesa Saad Shalaby, Profesa wa Uchumi wa Michezo na Nuno Cardoso, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Klabu ya Sporting Lishpona na Salem Al Habsi, Rais wa Shirikisho la Ghuba kwa vyombo vya habari vya michezo.


 Kikao kijacho kitashughulikia marekebisho ya mwenendo huo kutoka kwa maoni na mikataba ya kisheria ambapo kitazungumzwa na Salvatore Chevalier, Rais wa Chama cha Wanariadha wa Michezo nchini Italia, Mohamed Al-Muhairi, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Chama cha Soka cha Emirates, Bernard Palmero, Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Sheria ya FIFA na Dokta Manal Bazadough, Rais wa jumuyia ya Jordani kwa utamaduni wa michezo.

 Kikao cha sita kitajadili jukumu la vyombo vya habari vya michezo katika Kuunga mkono kurudishwa kwa shughuli hiyo, Hayati Merlo, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Uandishi wa Habari, Fawaz al-Sharif,naibu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Kiarabu la Utamaduni wa Michezo, Hassan Sharara, Rais wa Shirikisho la Lebanoni la Utamaduni wa Michezo, Abdel Latif al-Mutawakkil, Rais wa Jumuiya ya Morocco ya Waandishi wa Michezo, na Mohamed Ismail, mjumbe wa Kamati ya kiutendaji ya Baraza la Michezo la Kiarabu, watazungumza .Na mkutano huo unamalizikiwa na hutoba kutoka kwa  Dokta Ashraf Sobhy  kisha kutangaza mapendekezo.

Comments