Waziri wa vijana na michezo ya kimisri :- uwezo wa vijana wa Afrika walisukuma kuelekea enzi mpya ya maendeleo na ustawi

Na alisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa unajali vijana wa ubunifu wa Afrika na kuheshimu mawazo yake chanya juu ya kukuza na kuimarisha bara la Afrika .

Dokta Ashrf Sobhy waziri wa vijana na michezo alisisitiza kwamba wizara inafanya juu chini ili kuimarisha jukumu la Misri la kutekeleza maoni ya pamoja ya kiafrika na kukuza mahusiano pamoja na raia wa Afrika kutokana na maoni ya uongozi wa kisiasa na kusambamba na kumbukumbu ya kuanzishwa kwa shirika la Umoja wa Afrika .


Sobhy aliongeza kuwa  wizara inatekeleza mipango, mikutano , programu , warsha na shughuli kadhaa  zinazolenga kuimarisha ushirikiano na mawasiliano kati ya ndugu  wa kiafrika tena kuimarisha sekta ya kuwawezesha vijana na kuongeza uzoefu wao katika uwanja wa uongozi , kukata maumuzi na kufanya kazi katika kwa kuwekeza nguvu za vijana na uvumbuzi wao , jambo  linaloshirikisha kwa ufanisi katika kuboresha na kuendeleza sekta za kiuchumi zote  barani Afrika , kwa kuwazingatia mojawapo ya urasilimali na uwezo wa bara ili kukabiliana changamoto zote na kufikia matarajio na matumaini ya raia wake .


Aliendelea kusema kuwa nchi ina imani kwamba nguvu kubwa ya vijana wa Afrika inaweza kusukuma bara kwa enzi mpya ya maendeleo na ustawi na kufanya kazi ili kutekeleza mpango wa Umoja wa Afrika kwa mwaka  2063 kwa kusambamba na mpango wa maendeleo ya kudumu 2030 , akiashiria kuwa Rais Abd el-Fatah El-sisi anajali mawazo mazuri na ubunifu wa vijana wa bara la Afrika wanaolisukuma mbele kwa maendeleo na uboreshaji. 


Waziri wa michezo alisisitiza umuhimu wa shughuli ya michezo katika kuunda vizazi wanaoweza kubeba jukumu na kuendeleza bara .

Misri inatilia mkazo wa kukaribisha shughuli  kadhaa za michezo za kirafiki  na kufanya mikutano kwa mahudhurio ya wana wa bara la Afrika ili kuunga mkono viungo vya utamaduni na kiustaarabu kati ya raia wetu ili kuthibitisha utambulisho wa kiafrika na kuangazia misingi ya ushirikiano wa kiafrika na kusisitiza kwa jukumu la Misri la upainia sasa hivi na mipango ya ushirikiano yenye manufaa kati ya Misri na nchi nyingi za kiafrika  katika nyanja mbalimbali .

Comments