Baraza la kiarabu la maswala ya haki za binadamuLaanzisha kamisheni ya kiafrika isiyo ya kiserikali ya maswala ya wakimbizi
- 2019-05-30 13:10:11
Baraza la kiarabu la maswala ya haki za binadamu limefanya
warsha ya kikanda ya kiafrika ili; kujadili na kuonesha uhalisi wa changamoto zinazowapambana wakimbizi na wahamiaji wa kiafrika. Na hayo
yote yanakuja kulingana na mikutano ya kikao cha 64 cha tume ya kiafrika
ya maswala ya haki za binadamu na raia
mjini Sharm EL-Shekhi.
Mkuu wa baraza la kiarabu la maswala ya haki za
binadamu Bwana Ahmed Abdl Gawad ameeleza kuanzisha kamisheni ya kiafrika
isiyo ya kiserikali ya maswala ya
wakimbizi. Aisisitiza kwamba lengo la
warsha hiyo ni kuanzisha utendaji bora
na jaribio la baraza la kiarabu linalohusu kutoa ulinzi na usaidizi wa
kisheria kwa wakimbizi na wahamiaji.
Na ameongeza kusema
pia lengo la warsha hiyo ni kuonesha uhalisi wa changamoto za wahamiaji na
wakimbizi barani Afrika, mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika
kuimarisha juhudi zote zinazotolewa kwa Umoja wa kiafrika na tume ya kiafrika
chini ya uongozi bora wa kimisri kwa
kikao cha 64 cha tume ya kiafrika ya maswala ya haki za binadamu na raia.
VileVile amefafanua kuwa juhudi na uangalifu wa uongozi wa
kimisri kwa kikao cha 64 cha tume ya kiafrika ya maswala ya haki za binadamu na
raia zilisababisha kuzingatia mwaka wa 2019
ni mwaka wa wahamiaji barani Afrika .
Inatajwa kuwa shamrashamra rasmi za kikao cha 64 cha tume ya
kiafrika ya maswala ya haki za binadamu na raia zimeanza siku ya Jumatano iliyopita
mjini Sharm EL-Shekhi kwa kushiriki wakilishi wote wa tume hiyo, wakilishi wa
kamati kuu ya umoja wa kiafrika, Ujio wa makumi ya mataifa ya kiafrika,jumbe za
kideplomasia za kigeni , mashirika ya umoja wa mataifa maalumu, taasisi 35 za
kiraia za maswala ya haki za binadamu na
zaidi ya mashirika 100 yanayohusu Haki na
yasiyo ya kiserikali ya kiafrika ya kimataifa yakiwemo mashirika 12 ya
kimisri.
Comments