Kwa mara ya kwanza ... Vijana na Michezo yazindua program ya moja kwa moja kwa Kiingereza Alhamisi ijayo
- 2020-06-01 16:21:02
Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana wa kiafrika - Idara kuu ya Programu za Kitamaduni na kujitolea) inajiandaa kuzindua kipindi cha kwanza cha Programu ya Mwananchi wa Ulimwenguni siku ya Alhamisi, 4 Juni 2020.
Inatarajiwa kuvitangaza vipindi hivyo moja kwa moja kwenye ukurasa rasmi wa Wizara ya Vijana na Michezo, ukurasa wa Ofisi ya Vijana wa Kiafrika, ukurasa wa Vijana wa Nasser, ukurasa wa mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika na ukurasa wa mradi wa kielimu wa Mibegu pamoja na YouTube.
Orodha ya wageni wa programu hiyo ni pamoja na idadi ya watoa maamuzi na viongozi wachanga kutoka nchi tofauti za ulimwengu na katika nyanja tofauti kadhaa , ikilenga kueneza ujumbe chanya kwa vijana wa ulimwengu kutoka kwa Kairo na pia kuwaunganisha vijana na watoa maamuzi, inayochangia kuandaa viongozi wa vijana wenye uwezo wa kufanya mabadiliko yanayoonekana kiutendaji.
Programu hiyo inakuja kulingana na mkakati wa Wizara ya Vijana na Michezo, inayohangaika kuwawezesha vijana na kuimarisha jukumu lao kukabili misiba ya kimataifa, ikiamini katika uwezo wa vijana kukabiliana na misiba ile kupitia shughuli , harakati na mipango kadhaa ya kuingiliana.
Vipindi vya Programu hiyo vinashikiliwa na Amira Sayed, mwandishi wa habari kwenye Gazeti la El Egyptian Gazet , linalozingatiwa gazeti la kwanza linalotamka kwa Kiingereza kwenye Mashariki ya Kati, pamoja na yeye ni mwakilishi wa Misri katika Bunge la Vijana la Kimataifa kwa Maji na ameshiriki katika matukio kadhaa ya kimataifa ndani na nje ya Misri.
Comments