Waziri wa Vijana na Michezo aongoza Wibennar ya kwanza katika uwanja wa ujasiriamali na kazi za siku zijazo kwa kuzingatia changamoto za COVID-19

Wizara ya Vijana na Michezo kwa Vijana iliandaa kwa vijana wibennar  ya kwanza katika uwanja wa ujasiriamali na kazi za baadaye chini ya anwani ya "ujasiriamali na kazi za siku zijazo kwa kuzingatia changamoto za COVID-19" chini ya usimamizi na kuwepo kwa Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo, kwa kuzingatia mkakati wa wizara hiyo kuelekea mafunzo na uwezeshaji wa vijana Wamisri na jukumu lao kwao Na hamu yake ya mara kwa mara ya kuwaunga mkono wakati wa hali za kisasa .


Sobhy aliongoza kikao cha kwanza cha majadiliano ya kielektroniki na ushiriki wa watu mashuhuri wa ujasiriamali na wataalam wa miradi midogo akiwemo Dokta Ghada Ali profesa wa usimamizi wa biashara, mhandisi Ahmed Othman rais wa Baraza la Kimataifa la miradi midogo , Dokta Mohamed Azam Mshauri wa mabadiliko ya dijiti , Dokta Wael Eldosoky Meneja wa vituo vya ujasiriamali katika chuo cha kiarabu, Dokta Nizar Samy mshauri wa ubunifu na ujasiriamali na Ahmed Farag Meneja wa kimataifa wa masuluhisho ya Sekta ya Serikali na Mabadiliko ya Dijiti - Microsoft.


Kikao hiki kinakusudia kuchambua fursa na changamoto ambazo vijana kwa ujumla wanazikabili katika kujiunga kwao na ajira mpya zilizoundwa katika siku zijazo na pia kutoa masuluhisho kwa shida zinazowakabili wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwa sasa na kuwasaidia waendelee kufuatia changamoto za virusi vya Corona.


Sobhy alifafanua kuwa Wizara ya Vijana inachukua jukumu zuri la kiutendaji katika uwanja wa  kutoa mafunzo kwa vijana juu ya ustadi unaohitajika kwa kazi za mustakabali zisizo za jadi na ujasiriamali na miradi midogo, kwani sekta ya miradi midogo  inawakilisha umuhimu mkubwa katika uchumi wa nchi, na lazima tupanuke katika kusaidia vijana katika hatua zao za kwanza za kuongoza miradi inayoibuka na hatari ya kuhesabiwa na  Masomo sahihi ya ratiba . 


Sobhy aliongezea kuwa ujasiriamali una jukumu kubwa katika uchumi wa nchi kwa sababu huunda fursa mpya za kazi na huleta bidhaa mpya na maoni katika soko .. Bila maoni ya ubunifu wa wajasiriamali, ulimwengu wetu haungekuwa wa hali ya juu kama ilivyo leo katika nyanja za utamaduni, sayansi na teknolojia.


Akionyesha kuwa Wizara inatoa fursa nyingi za kuwezesha na kukuza uwezo wa kiteknolojia na wa ubunifu kwa vijana na akawasihi kushiriki katika kambi za kawaida ili kuunda maoni ya ubunifu kupitia hatua ya viongozi wa vijana kuwafikia vijana kutekeleza mawazo ya mradi, basi Wizara itachukua jukumu lake katika kuwapa mtandao na watengenezaji wa biashara , pamoja na hitaji la kuwekeza vijana Kwa wakati huo hasa mnamo kipindi cha marufuku kwa kuungana na semina bure za wizara katika mpango wa "TAWAR" ambao unawawezesha vijana kwa kazi za kisasa kama vile biashara ya kielektroniki na uuzaji wa kielektroniki , kuandaa maelezo katika dijiti na kufafanua hadhira inayolenga katika ukweli wa dijiti na ujuzi mwingine wa kisasa wa kiteknolojia, hii ni pamoja na mpango wa Benki ya kielektroniki ambayo inatoa Zaidi ya ajira 1000 kwa wiki kwenye tovuti rasmi ya Wizara na ukurasa wake wa Facebook.


Sobhy alipendekeza umuhimu wa kurudia mikutano kama hiyo ya kielektroniki na vijana na wataalambkatika ujasiriamali na miradi midogo ili kujadili mambo yote ambayo ni mapya , kujibu maswali ya vijana na kujibu wasiwasi wao katika hali za kisasa, na aliwataka vijana kupeana maoni yao na maombi ya mafunzo na mawasiliano endelevu ya kielektroniki na Wizara.

Comments