Waziri wa Vijana na Michezo asifu mapendekezo ya mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Utamaduni wa michezo

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana wa na Michezo wa Misri, Mwenyekiti wa Ofisi ya kiutendaji ya Baraza la Vijana na Mawaziri  waarabu wa Michezo, alisifu mapendekezo ya mkutano wa tatu wa kimataifa ulioandaliwa na Shirikisho la Utamaduni wa Michezo unaoongozwa na  Mtangazaji wa vyombo vya habari Ashraf Mahmoud, Rais wa Shirikisho la Kiarabu la Utamaduni wa Michezo, uliofanyika kwa muda wa siku 3 na ushiriki wa kikundi chake cha viongozi wachezaji wa Kiarabu, wa Kiafrika na wa nje waiiwakilisha nchi 18, na mkutano huo uliofanyika kupitia "Video Conference" ... chini ya kauli mbiu "Kurekebish njia kwa ajili ya mchezo  wa usalama ulimwenguni."


Waziri huyo alilishukuru Shirikisho la Misri kwa Utamaduni wa Michezo kwa kufanikiwa kwa mkutano huu, ambao aliona ni ya kwanza ya aina yake, na alama kubwa za michezo kutoka ulimwengu wa Kiarabu na Afrika zilishiriki ndani yake, akisisitiza kuwa kila wakati alikuwa akijivunia kuwa mmoja wa waanzilishi wa tamaduni ya michezo kwani ilikuwa ni ya kiraia hadi ikuwa muungano wakati wa Mhandisi Hassan Sakr, Rais wa zamani wa Baraza la Michezo la kitaifa.


Dokta Ashraf Sobhy alielezea furaha yake na mapendekezo hayo, kwani yalipatikana ukweli na kuelezea uzoefu wa wahadhiri na yanatekelezeka, akisisitiza kwamba atawasilisha kwa mawaziri waarabu wa vijana na michezo mwanzoni mwa fursa ya kuzitekeleza ardhini.


Dokta Imad Al-Bennani, mkuu wa zamani wa Baraza la Michezo , na rais wa Shirikisho la Kiarabu kwa mashirikisho ya Michezo ya anuai, alitangaza siku ya alhamisi  mapendekezo 15 ya mkutano huo ulioanza Jumanne iliyopita . Mapendekezo maarufu zaidi yalikuwa ya kukata rufaa kwa serikali kutoa msaada wa kifedha kwa mashirika ya michezo na klabu kuunga mkono kukabiliana na uharibifu wa uchumi uliosababishwa Juu ya janga la virusi vya Corona, pamoja na maendelezo ya ushirikiano kati ya mashirika na klabu kuhakikisha kurejesha usalama kwa mashindano mbalimbali na utekelezaji wa makubaliano yote ya matibabu kwa mujibu wa viwango vya matibabu na mahitaji yaliyotangazwa na Shirika la Afya Ulimwenguni, na umuhimu wa kubuni mbinu mpya za uuzaji wa michezo, kuunda hali mpya ya uchumi wa kiuchumi ... Kwa kushirikiana na vyombo vyote vya habari.


Siku ya mwisho ya shughuli za mkutano huo zilishuhudia mkutano wa  "Marekebisho ya kisheria na mikataba" ambapo: Dokta Manal Bazadough, Rais wa Jumuiya ya Tamaduni ya Michezo, Slivatori Chevalli, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Italia, na Bernardo Palmero, mkurugenzi wa zamani wa Chama cha Soka cha Kimataifa FIFA, walizungumzia, Pamoja na na Ahmed Abd El Fatah wa Misri, mjumbe wa Shirika la Kimataifa la Michezo,  wakikubaliana kwamba janga la Corona bila shaka litabadilisha utaratibu wa makubaliano kati ya vilabu na wachezaji katika michezo yote, na kati ya klabu na mashirika ya michezo na makampuni ya kibiashara yanayowafadhili, kwa kuzingatia uwezekano wa upungufu mkubwa wa thamani  ya mikataba na thamani ya udhamini.


Mwishoni  mwa mkutano huo, Mtangazaji bwa vyombo vya habari Ashraf Mahmoud, Rais wa Shirikisho la Michezo la Utamaduni la Misri alitangaza kwamba kipindi kijacho kitashuhudia semina maalum na nchi za Kiarabu kubadilishana uzoefu katika uwanja wa michezo na itakuwa ya kwanza wiki ijayo na Shirikisho la Palestina kwa Utamaduni wa Michezo.


Comments