"Ubunifu na kusaidia uwajibikaji wa kijamii kwa Mustakbali bora zaidi baadaye" kilikuwa kipindi cha kwanza cha Programu ya Mwananchi wa kimataifa
- 2020-06-08 19:39:46
Alhamisi iliyopita,kipindi cha kwanza cha Programu ya Mwananchi wa Ulimwengu ikidhaminiwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya kiafrika - Idara kuu ya Programu za kiutamaduni na Hiari) kwa kichwa cha "Ubunifu na kusaidia Uwajibikaji wa kijamii kwa Mustakbali bora zaidi baadaye".
Programu hiyo ilianza kipindi chake cha kwanza kwa kumkaribisha kijana wa Uhispania wa miaka 31, Carlos Sentis, mwanzilishi wa Taasisi ya "World Impact Alliance", mwanachama wa timu ya Jukwaa la Uchumi wa dunia na mhadhiri wa vyuo vikuu zaidi ya saba vya ulimwengu.
Mwanzoni mwa mkutano, Santis alielezea furaha yake kwa kushiriki katika Programu ya Mwananchi wa Ulimwengu, na alionyesha umuhimu wa mipango kama hiyo katika kusaidia lugha ya mazungumzo na mawasiliano kati ya vijana katika nchi tofauti za ulimwengu. Akizungumzia athari za virusi vya Corona, Santis aliashiria kuwa marufuku ni kipindi cha kujitambua tena na aliwaomba wote kutumia vizuri kipindi hiki na alithibitisha kwamba anafuata kwa karibu mabadiliko ambayo yamejitokeza katika sekta zote katika nchi tofauti za ulimwengu baada ya mlipuko wa janga la Corona.
Akizungumzia Taasisi ya " World Impact Alliance", Santis alisisitiza kwamba lengo kuu la taasisi hii ni kuimarisha uwajibikaji wa kijamii kwa makampuni na taasisi katika sekta mbili za umma na za kibinafsi kupitia mashirikiano kadhaa na serikali tofauti, Jumuyia za kiraia na Vyombo vya habari. alieleza kuwa njia ya kufikia lengo hili sio rahisi, lakini sio haiwezekani.
Wakati wa mkutano, Santis alizungumzia safari zake ulimwenguni na ziara zake kwa zaidi ya nchi 30, na akasisitiza kwamba linalotutunganisha ni zaidi ya lile linalotutenganisha. Pia alizungumzia ziara yake ya hivi karibuni nchini Misri wakati wa kushiriki kwake katika toleo la tatu la Mkutano wa Vijana wa Ulimwengu chini ya Uangalifu wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, na alielezea furaha yake kubwa kwa kuongea na Rais El-Sisi katika moja ya vikao vya mkutano huo na kusisitiza umuhimu wa kuunda kiunga cha mawasiliano kati ya vijana na watoa maamuzi.
Mwishoni mwa mkutano, Santis alipeleka ujumbe kwa vijana wa nchi tofauti za ulimwengu, akiwahimiza kuwasaidia wengine na kuwa na nguvu zaidi na kufurahi hali chanya za maisha, pia aliwahimiza wajigundue, kukuza ujuzi wao, na kuacha alama wazi.
inapaswa kutaja kuwa mkutano huo ulitangazwa moja kwa moja kwenye kurasa za mawasiliano ya kijamii za Wizara ya Vijana na Michezo, Ofisi ya Vijana ya Kiafrika, Harakati ya Vijana wa Nasser, Mfumo wa kuiga Umoja wa Afrika na Taasisi ya Vijana ya Afrika-Asia.
Programu hiyo inazingatiwa programu ya kwanza ya moja kwa moja kwa Kiingereza iliyozinduliwa na Wizara , kwa lengo la kusaidia dhana ya umoja na ushiriki wa ulimwengu, na pia kuangazia uzoefu wa kimataifa wa vijana wenye mafanikio.
Orodha ya wageni wa programu hiyo ni pamoja na idadi ya watoa maamuzi na viongozi vijana kutoka nchi tofauti za ulimwengu na katika nyanja tofauti , kwa lengo la kueneza ujumbe chanya kwa vijana wa ulimwengu kutokana na Kairo, pia na pia kuwaunganisha vijana na watoa maamuzi, linalochangia kuandaa viongozi vijana wenye uwezo wa kufanya mabadiliko yanayoonekana wazi.
Comments