Waziri wa Vijana na Michezo: " kubaki makao makuu ya CAF nchini Misri ni dalili ya uongozi wetu na jukumu letu la kihistoria barani "

Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alithibitisha kwamba udhibitisho wa Bunge ulioongozwa na Dokta Ali Abd El Aal wakati wa kikao chake cha Jumatatu kuhusu idhini ya makubaliano ya makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika kati ya Misri na Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika ni uthibitisho na dhamana ya jukumu la Misri la upainia na la kihistoria barani Afrika.


Dokta Ashraf Sobhy aliongeza kwamba makubaliano hayo mapya yanakuja kama mbadala wa makubaliano ya makao makuu yaliyotangulia mnamo Novemba 2007 kati ya pande hizo mbili, hasa baada ya makubaliano ya awali yanamalizika, CAF iliwasilisha ombi la kutia saini makubaliano mpya ya makao makuu.


Baraza la Wabunge wakati wa kikao chake cha umma  kilichoongozwa na Dokta Ali Abd El Aal lilikubali uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Misri, Namba 149 ya 2020 ya kupitisha makubaliano ya makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu la Kiafrika kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Shirikisho la Mpira wa Miguu la kiafrika.


Hii ilikuja wakati wa kikao cha Bunge , ambapo makubaliano yanalenga kuendelea kusaidia shughuli na juhudi za CAF ili kuwezesha mchango wake wa kukuza, kueneza  na kuboresha umaarufu wa mpira wa miguu barani Afrika.


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alichukua jukumu kubwa katika kuhitimisha makubaliano ya kukaribisha tena kwa Misri kwa makao makuu ya CAF kwa kipindi cha miaka 10 baada ya hali  ya mabishano iliyodumu kwa miezi kadhaa kutokana na hamu ya maafisa wa Umoja wa Afrika kuhama makao makuu kutoka Misri, lakini Dokta  Ashraf Sobhy kwa msaada wa Nchi ya Misri alifanya bidii na alikuwa mkali katika Kongamano la CAF lililofanyika nchini Misri 2019, akisisitiza hitaji la makao makuu ya CAF kubaki nchini Misri, na kusisitiza kwamba serikali ya Misri ilipeana njia zote za faraja kwa maafisa wa Umoja wa Afrika kwa makao makuu kubaki nchini Misri, akielezea kuwa hakuna uzembe  katika faili hili kamwe.


Waziri wa Vijana na Michezo alizidisha juhudi zake katika kipindi cha mwisho kwa kuzungumza na shirikisho la mpira wa miguu la kimataifa (FIFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika ili kukamilisha taratibu zote za makubaliano ya makao makuu ya CAF na kudumisha kuwepo kwake nchini Misri, akithibitisha jukumu la upainia la Misri katika barani Afrika.


Ripoti ya Kamati ya Vijana na Michezo ilisema kwamba makubaliano yaliyowasilishwa ni dhibitisho la jukumu la kihistoria la Misri kama mojawapo ya nchi zilizoanzisha Shirikisho la Soka la Afrika, lililosababisha  kukaribisha kwake kwa makao makuu ya Shirikisho huko Kairo, ambayo ni nyongeza ya msimamo wa upainia wa Misri barani Afrika sio tu katika ngazi za kisiasa, kijamii na kitamaduni , bali ya kimchezo pia . Hasa katika uwanja wa mpira wa miguu kwani Misri ilikuwa nchi ya kwanza iliyoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mnamo 1957, na pia inasajili rekodi ya kushinda kombe hilo mara saba.


Kamati husika ilithibitisha kwamba hitimisho la makubaliano haya linathibitisha dhamira ya Misri kutoa vifaa vyote kwa makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika na kwamba kumekuwa na juhudi za serikali ya Misri kushughulikia majaribio ya kuhamisha makao makuu ya CAF nje ya Misri katika mfumo wa mpango wa serikali wa kusaidia makao makuu ya mashirikisho ya kimataifa nchini Misri kwa kutenga bajeti na kutoa vifaa vyote, hasa tangu kuwepo kwa makao makuu ya Umoja wa bara unawakilisha nyongeza yenye nguvu na kuimarisha uchumi pamoja na kukuza utalii na faida kadhaa muhimu.


Inatajwa  kuwa serikali ya Misri ilimaliza mabishano hayo mnamo Februari iliyopita kuhusu uwezekano wa kuhamisha makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika "CAF" kutoka Kairo, ambapo Waziri Mkuu Dokta Mostafa Madbuly alihudhuria sherehe ya kusainiwa makubaliano kuhusu kukaribisha tena kwa Misri kwa makao makuu ya CAF kwa muda wa miaka 10 na itafanywa upya moja kwa moja kati ya Misri na Shirikisho la Soka la Afrika, makubaliano hayo yalitiwa saini na Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo na Ahmed Ahmed Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika.


Kwa upande wake, Kamati ya Vijana na Michezo ilithibitisha shukrani zake za kina kwa Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo kwa juhudi zake za kuhifadhi makao makuu ya shirikisho la Afrika nchini Misri na kutimiza makubaliano haya.

Comments