Senegal inaongoza bara la Afrika ... Timu ya kitaifa ya Misri ni ya saba barani katika uainishaji wa " FIFA" wa kila mwezi

Alhamisi, Shirikisho la kimataifa la Soka " FIFA"  lilifungua pazia mbele ya uainishaji wa kila mwezi kwa timu ya taifa ya wanaume 


Na timu ya kitaifa ya Misri ilifikia nafasi ya 51 ulimwenguni , wakati ambapo ilifikia nafasi ya saba barani Afrika .


Uainishaji mpya haukushuhudia mabadiliko yoyote ikilinganisha kwa uainishaji uliopita  uliotolewa tarehe 9 mwezi wa Aprili  uliopita kwa sababu kutocheza mechi.


Shida ya kiafya kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona bado ni kizuizi mbele ya kuandaa mechi za kimataifa kati ya timu za kitaifa licha ya kurudi kwa idadi ya mashindano ya michuano za ligi ulimwenguni hatua kwa hatua.


Timu ya kitaifa ya Ubelgiji iliendelea  kupatikana mbele ya uainishaji .


Uainishaji wa waarabu watano wa kwanza ulikuja kama yafuatayo :-


Tunisia (27) , Algeria (35), Morocco(43) , Misri (51),  Qatar(55) .


Uainishaji wa watano wa kwanza barani  Afrika ulikuja kama yafuatayo:-


Senegal(20) ,  Tunisia     (27) ,  Nigeria(31), Algeria (35)  ,  Morocco(43) .


Uainishaji wa watano wa kwanza katika Asia ulikuja kama yafuatayo :-


 Japan (28), Iran(33),Korea kusini (40), Australia (42),  Qatar(55) .


Comments