Kuanza hatua za tahadhari ili kujiandaa kurudi tena shughuli ya kimichezo

Kamati ya juu ya usimamizi wa janga la  "Corona" kwa uongozi wa Madbuly inaamua: 


Kuendelea Marufuku ya harakati za raia kutoka saa 2   usiku hadi saa 10  asubuhi kuanzia 14 mwezi wa Juni hadi mwisho wa mwezi huo. 


Kusimamisha harakati za usafirishaji wa umma kuanzia saa 2  usiku na kuendeleza 

Kufunga mabustani ya umma na pwani.



Na lazima kila waziri achukue uamuzi wa usimamizi kuhusu kupunguza idadi ya wafanyakazi kutokana na hali ya kufanya kazi katika wizara yake.  


Kuruhusu kwa vilabu vya kimichezo kwa kuanza kupokea Uandikishaji wa wanachama na kuboresha ufanisi wa majengo kutoka 15 hadi 30 mwezi huu wa Juni.


Kujadili ufunguzi wa mahali pa ibada kuanzia  mwezi wa Julai

Katika mikoa inayoambukizwa kwa virusi vya " Corona " kwa idadi ndogo kabisa kutokana na kuendeleza msimamo wa kiafya na Kujitolea kwa raia.


Kutangaza mnamo mwanzo wa mwezi wa Julai kwa kuanza utalii na usafirishaji wa anga katika mikoa ya kiutalii yenye idadi ndogo kabisa ya kuambukizwa kwa virusi vya " Corona "


Kamati Kuu ya Usimamizi wa Mgogoro mpya wa virusi vya Corona ilifanya mkutano wake asubuhi ya leo katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri iliyoongozwa na Dokta Mustafa Madbuly Waziri Mkuu kupitia teknolojia ya mkutano wa video, ambapo ilikagua juhudi za kukabili virusi vipya vya Corona, na hali ya kesi za maambukizi na kupata nafuu, pia kuonyesha mipango ya wizara mbalimbali zinazohusika ili kuzifungua pole pole kulingana na maendeleo katika hali ya afya nchini.


Mshauri Nader Saad, msemaji rasmi wa Baraza la Mawaziri alisema kwamba iliamuliwa kuendelea kupiga marufuku harakati za wananchi kuanzia saa 2 usiku hadi saa 10 asubuhi kuanzia Jumapili ijayo siku ya 14 mwezi wa Juni hadi Jumanne siku ya 30 na pia kukomesha harakati za usafiri wote wa umma kutoka kwa 8 usiku kila siku na upanuzi wa kazi ya maduka  makubwa kwa saa moja ili kumalizika saa 12 usiku badala ya 11 kwa kipindi chote hicho na kuendelea kwa kufungwa kwa mabustani ya umma na fukwe za umma hadi mwisho wa mwezi huu.


Mshauri Nader Saad ameongeza: Pia iliamuliwa kuendelea na uamuzi uliopita wa Waziri Mkuu wa kupunguza idadi ya wafanyakazi katika wizara na mashirika ya serikali Ili kuzuia mchanganyiko na fuleni na kile waziri anatakiwa kuchukua maamuzi ya kiutaratibu kuandaa hivyo kulingana na hali ya kazi katika wizara yake pamoja na kuruhusu vilabu vya michezo kuanza kupokea michango kwa wanachama kuanzia siku ya 15 mwezi wa Juni hadi 30 mwezi wa Juni  pamoja na kuongeza ufanisi wa majengo na kuyarekebisha tena katika wakati huo.


Msemaji rasmi wa Baraza la Mawaziri alisema: Kamati hiyo pia iliamua kusoma ufunguzi wa mahali pa ibada kuanzia mwanzo wa Julai kwa awali katika mikoa yenye idadi ndogo kabisa iliyoambukizwa virusi vya Corona  na kulingana na maendeleo ya hali ya kiafya na kulingana na kiwango cha dhamira na kujitolea kwa wananchi kufuata hatua za amani na kinga ya afya iwapo hali ya kufungua na kutafakari tena hali hiyo moja kwa moja .


Alisema kuwa iliamuliwa kutangaza mwanzo wa Julai ijayo harakati za utalii zinazoingia na safari ya ndege kwa mikoa ya watalii yenye idadi ndogo kabisa ya kuambukizwa na virusi vya Corona ambayo ni Sinai kusini, Bahari Nyekundu na Matrouh, akisisitiza makubaliano ya Kamati Kuu ya kudhibiti mgogoro wa "Corona" kushikilia mitihani ya wanafunzi wa shule za sekondari kama ilivyopangwa kabla, kulingana na udhibiti na masharti ya afya yaliyokubaliwa na kuyafuata kila siku ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi  watoto wetu.

Comments