Tangu mwanzo wa Corona ... Wavulana na wasichana milioni 10 watumia programu za wizara ya vijana na michezo ya kimisri kwenye intaneti
- 2020-06-15 14:00:28
Wizara ya vijana na michezo ilihesabu idadi ya vijana wanaotumia programu na mipango iliyotekelezwa na wizara kwenye ukurasa wake rasmi kupitia tovuti za mawasiliano ya kijamii na kwenye lango la kielektroniki ambapo idadi zao zilikuwa vijana milioni 10 kutoka mikoa yote .
Wizara ya vijana na michezo ilikuwa ikitoa programu za intaneti moja kwa moja katika mfumo wa kupambana na virusi vya Corona kama kugundua vipaji vya kimisri (Shabaab w Talaae) , na mpango wa (Maak online) uliojumuisha" shindano la jua nchi yako , shindano la soma na shinda , semina za kazi katika nyanja za kisanaa " , pia mpango wa Ramadhani yako ni online unaojumuisha " shindano la utafiti juu ya habari za mtume , shindano la imba nyumbani mwako na shindano la swali na tuzo "
Wizara ya vijana na michezo ilitekeleza Logo ya mji mkuu mpya , na mpango dhidi virusi vya Corona , mpango wa mpango bora zaidi wa ugunduzi , na semina za kazi za kiufundi , na mlolongo wa mazungumzo ya Maak kwenye intaneti , na kuwezesha mipango ya vijana , na programu za makundi ya kufundisha ya kielektroniki , pia mipango ya " Matwafsh Faan , Faan mn El Balakona, Afshat Aflam " na mashindano kama " Samaana Sotak, Zaman ElFan ElGamil, Dijital Art," na shindano la kuhifadhi Quran , na mpango wa kuwaelemisha vipofu na bubu dhidi ya virusi vya Corona , vilevile tangazo la matokeo ya sherehe ya ubunifu wa msimu wa nane " .
Dokta Ashraf Sobhy alieleza kwamba wizara ya vijana na michezo inaendelea kutekeleza mfululizo wa mipango na programu kwa watoto na vijana wakati wa kubadilisha kwa digitali kwa shughuli na programu za wizara , akiashiria kuhangaika kwa ushiriki wa idadi kubwa ya vijana katika programu mbalimbali za wizara .
Waziri wa vijana alisifu ushiriki mzuri wa watoto na vijana katika mipango na mashindano na programu za wizara za online tokea mwanzo wa janga la Corona , na hivyo kupitia lango la kielektroniki la wizara na kurasa za mawasiliano ya kijamii , akiashiria kuwa kutathmini kwa programu zilizofanyika online mara kwa mara , na kujua matokeo yake na asilimia za ushiriki wake .
Comments