Waziri wa Michezo ajadili matayarisho ya Misri kwa ajili ya Mashindano ya Mpira wa mikono Duniani pamoja na kamati iandaayo
- 2020-06-16 14:53:08
Mitazamo ya sherehe za Kura na ufunguzi wa Kombe la Dunia la mpira wa mikono .. tiketi za mechi .. hatua za malazi na maisha .. Vitu maarufu zaidi vinavyojadiliwa katika Mkutano wa Waziri wa Michezo na Kamati iandaayo ya Kombe la Dunia la mpira wa mkono.
Dokt Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo, wakati wa mkutano wake na Kamati iandaayo ya Mashindano ya Mpira wa Mikono Duniani 2021 alijadili maandalizi yote yanayohusiana na kukaribisha Misri kwa mashindano hayo mwezi wa Januari ujao na ushiriki wa timu 32 za kitaifa.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta Hussein Labib Mkurugenzi wa Kamati iandaayo ya mashindano hayo , wakurugenzi kadhaa wa kamati ndogo, kikundi cha viongozi wa Wakuu wa Wizara , wanachama wa Kamati iandaayo na maafisa wa Kampuni ya presentation na Kampuni ya Tiketi yangu.
Mkutano huo ulikagua taratibu zinazohusiana na kukamilisha kazi za ujenzi katika kumbi zilizofunikwa zilizokaribisha mashindano hayo kwa nyakati maalum na kuziwasilisha katika mwezi wa Oktoba ijayo na kujadili pia hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa kuhusu maelezo ya tiketi za ndege, malazi , maisha , uhamishaji kwa timu zinazoshiriki na wajumbe rasmi, na taratibu zote za mashindano hayo.
Mkutano huo ulijadili na maafisa wa Kampuni ya presentation maoni ya sherehe ya Kura ya Kombe la Dunia la mpira wa mikono itakayofanyika katika Jumba la Makumbusho la Ustaarabu wa Misri pamoja na sherehe za ufunguzi na za kufunga za mashindano hayo na kuzungumzia hatua za uratibu zilizopatikana na kampuni "Tiketi yangu" kuhusu idadi za tiketi za mechi na viwango vyake na kamati iandaayo hutoa kampuni ya "Tiketi Yangu" ratiba ya mechi zote ili kampuni kwa upande wake iweze kupeana dhana kamili na bei zilizopendekezwa za tiketi.
Kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy alionyesha ufuatiliaji wa kila wiki na Kamati iandaayo ya Kombe la Dunia la mpira wa mikono - Misri 2021 kuangalia michakato na maandalizi yote ya mashindano hayo , akiashiria kwa uratibu na mawaziri, wajumbe wa Kamati Kuu iandaayo ya mashindano hayo na viongozi husika ili Kujadili maelezo yote ya mashindano.
Waziri wa Vijana na Michezo alithibitisha dhamira ya kufanikiwa kwa mashindano hayo na kuipanga kwa njia itakayovutia ulimwengu; Kukamilisha mfululizo wa mafanikio ambao Misri inafanikiwa katika kukaribisha michuano mikubwa ya michezo ya kimataifa na hayo kulingana na misingi na uwezo za nchi ya kimisri zinazoiwezesha kwa hivyo.
Mkutano huo ulijumuisha uwasilishaji juu ya matokeo ya mikutano iliyofanyikwa na Kamati iandaayo pamoja na kamati ndogo ndogo katika kipindi cha mwisho ikijumuisha Kamati ya Fedha, Kamati ya wanaojitolea, Kamati ya IT, na Kamati ya kumbi na kukubaliana kuchukua hatua zote muhimu ili kuhakikisha kuratibu mashindano hayo katika kiwango cha juu zaidi.
Comments