Michuano ya dunia kwa wavulana wa michezo ya silaha nchini Misri itafanyika katika miadi yake 2021... Na kuahirishwa kwa michuano ya wazima hadi 2022
- 2020-06-16 14:56:25
Mkuu wa shirikisho la silaha, Abd Almoneem Alhusseny, amesisitiza kuwa michuano ya dunia ya wavulana wa silaha uliopangwa kuifanyika nchini Misri mnamo mwezi wa Aprili, mwaka wa 2021 itafanyika katika miadi yake iliyopangwa, bila mabadiliko yoyote.
Alhusseny amesema : "kuhusu michuano ya dunia kwa wazima iliyopangwa kufanyika pia nchini Misri mnamo mwaka 2021, imeahirishwa rasmi hadi mwezi wa Julai, mwaka wa 2022 ; hii kwa sababu ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 mnamo mwaka ujao 2021 baada ya kuiahirishwa kwa sababu ya virusi vya Corona".
Na Alhusseny amesisitiza kuwa shirikisho la kimataifa la silaha hivi karibuni limetuma barua rasmi kuhusu uamuzi wa kuahirisha michuano ya wazima mpaka msimu wa joto wa mwaka 2022, badala ya miadi yake ya awali , mnamo msimu wa joto 2021.
Mkuu wa shirikisho la silaha ameashiria kuwa uamuzi huo ulitarajiwa kuhusu michuano ya ulimwengu kwa wazima, baada ya kuahirishwa Tokyo 2020 mpaka 2021 ; kwa kuwa linalojulikana daima katika shirikisho la kimataifa la michezo hiyo kwamba kutofanyika michuano ya ulimwengu kwa wazima mnamo mwaka huu huu wa kikao cha michezo ya Olimpiki kinafanyika, kwa ajili ya kuwaruhusu wachezaji kufanya mazoezi na maandalizi, pamoja na kuzingatia tu katika mashindano ya Olimpiki.
Alhusseny ameongeza akisema : "Shirikisho la silaha linatayarisha katika wakati wowote ili kukaribisha na kuandaa michuano yoyote ya kimataifa au ya ulimwengu, hasa baada ya mafanikio ya pande zote ya Misri ya kuandaa michuano yote ya kimataifa ya Silaha, na hivyo kutokana na kauli ya wote".
Comments