Waziri wa Vijana na Michezo ashiriki katika mkutano wa mawaziri wa vijana waafrika kupitia mtandao wa video

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Jumatano, kupitia mtandao wa video ameshiriki katika shughuli za mkutano wa Kamati ya kiufundi ya Mawaziri waafrika wa Vijana na Michezo ili kuonyesha uzoefu wa nchi za Kiafrika na hatua za tahadhari zilizochukuliwa na serikali za Kiafrika katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona kuhusu taratibu na udhibiti wa kurudi tena shughuli za kimichezo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na kikundi cha mawaziri waafrika wa vijana na michezo kutoka nchi kadhaa, pamoja na "Sudan Kusini, Morocco, Algeria, Rwanda, Kongo Brazzville,na Zambia", Mjumbe wa Vijana kwenye Umoja wa Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF na Sekertareti Mtendaji wa Tume ya kiuchumi ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, na maafisa wengine.

Mkutano wa mashauriano wa vijana ni pamoja na vikao vya kazi vinavyozunguka mwitikio wa sekta ya vijana huko Umoja wa Afrika kwa kukabili virusi vya Corona na nafasi zinazojitokeza, fursa za kujenga uwezo kwa wizara za vijana wa Umoja wa Afrika, kuzindua mpango wa Ujuzi unaohusiana na kugharimia uvumbuzi barani Afrika, mazoea mazuri, kubadilishana uzoefu kutokana na wizara za vijana wa Umoja wa Afrika.

Katika uingiliaji wake, Dokta Ashraf Sobhy alitoa Jaribio la Kimisri la kukabiliana na mlipuko wa virusi vipya vya corona, kwa kuzingatia maagizo ya Rais Mheshimiwa Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri kwa kutia maanani afya na usalama wa Wamisri mwanzoni mwa vipaumbele, na serikali ya kimisri inayoongozwa na Dokta Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, imechukua hatua na fahamu za tahadhari, na kuzitekeleza katika pande zote za Jamhuri ili kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, na miongoni mwa maamuzi hayo ilikuwa ni kusimamisha shughuli zote za vijana na michezo kuzuia mikusanyiko na kupunguza mlipuko wa virusi.

Waziri wa Vijana na Michezo aliendelea akisema: " katika Wizara ya Vijana na Michezo tumefuatilia utekelezaji wa maamuzi yote yaliyochukuliwa na serikali ya kimisri katika nyanja za vijana na michezo, na njia za kiteknolojia zimetumika vizuri katika kutekeleza kikundi cha mipango na miradi ya watu wakubwa na vijana kwenye mitandao ambayo wameingiliana nayo hadi sasa, washiriki wa milioni 10, pamoja na Kutoa vituo vya vijana vilivyotawanyika kote nchini kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika muktadha wa kuzibadilisha na kuwa vituo vya huduma za jamii, pamoja na ushiriki wa vijana wamisri katika harakati za usafishaji na utakaso wa majengo vya vijana na michezo, vijiji na maeneo jirani".

Kuhusu kurudi tena shughuli za kimichezo, Dokta Ashraf Sobhy alisema kuwa serikali ya kimisri ilikubali kurudi tena shughuli za kimichezo, zitakazoanza mnamo Julai ijayo katika vituo vya vijana na vilabu vya michezo, kulingana na udhibiti maalum wa tahadhari na taratibu zitakazosambazwa kwa vituo vyote vimekabidhiwa kwao ili kuhifadhi afya na usalama wa wanariadha na wanachama wanaokuwepo kwenye vituo hivyo, akionyesha kuwa jambo hilo litafuatwa kwa kurudi tena shughuli hizo katika mfumo wa kutathmini na ufuatiliaji wa kesi zozote ambazo zinaweza kuonekana kuchukua hatua sahihi kuelekea jambo hilo.

Katika muktadha mwingine, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ya kimisri inatia maanani makubwa kwa wanafunzi waafrika wanaosoma nchini Misri, na inawapa mipango na miradi tofauti mnamo mwaka mzima , ikiamini kwamba wao ni viongozi wa siku zijazo katika nchi ndugu tofauti za Kiafrika, akiashiria hitaji la kushirikiana na mawaziri wote waafrika wa Vijana na michezo; kuweka mtazamo wa pamoja kwa maendeleo ya programu za kimichezo na vijana barani.

Comments