Waziri wa vijana ajadili na mwenyekiti wa mamlaka ya michezo ya kijeshi maandalizi ya kukaribisha Misri kwa michuano ya kombe la dunia la kijeshi la Soka 2021

 Katika maktaba ya Diwani ya  wizara, leo Jumatano, Waziri wa vijana na michezo, Dokta Ashraf Sobhy amefanya mkutano na jenerali Sabry Mosilhy,  mwenyekiti wa mamlaka ya michezo ya kijeshi ili kujadili matayarisho yanayohusiana na kukaribisha  Misri kwa michuano ya kombe la dunia la Soka la tatu la kijeshi - Misri 2021.


Michuano ya kombe la dunia la tatu la kijeshi ni michuano ya kwanza wa kombe la dunia la kijeshi katika toleo lake jipya itakayofanyika barani Afrika kwa ushiriki wa timu za kitaifa 16 ambazo ni : timu za kitaifa 4 kutoka kwa Ulaya, timu za kitaifa 4 kutoka kwa Afrika, timu za kitaifa 4 kutoka kwa Asia na timu za kitaifa 4 kutoka kwa Marekani mbili, pia iliyopangwa kucheza mechi za michuano kwenye viwanja vya mpira vya : ( Kairo, chuo kikuu cha kijeshi, ulinzi wa hewa, Alsalam, Petro Sport na mamlaka ya michezo ya vikosi vya silaha ), hii kulingana na mkataba wa ushirikiano ulisainiwa kwa mamlaka ya michezo ya vikosi vya silaha na baraza la kimataifa la michezo ya kijeshi. 


Waziri wa Vijana na Michezo ametarajia kufanikiwa kwa michuano hiyo ,  kwa kile ambacho Misri ina katika suala la kufaulu na upatikanaji wa viwanja vya mpira , hoteli za makazi, hospitali, vitu vya bima na uhamishaji, akiashiria utumiaji wa viwango bora vya ushirikiano kwenye kiwango cha kuandaa michuano hiyo kwa njia bora na sahihi kwa Kombe la Dunia la kijeshi la Soka. 

 

Mkutano huo pia umejadili ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Mamlaka ya Michezo ya Kijeshi,  wakati ambapo jenerali Sabri Moshehli akionesha mafanikio ya shule za michezo za kijeshi nchini Misri, ambazo ni pamoja na shule 6 ambazo ziliweza katika kipindi cha nyuma kushinda medali 30,000 kwenye kiwango cha ubingwa wa kitaifa nchini, medali elfu 3 za Kiarabu na Kiafrika na medali 300 za kimataifa. Na hivyo katika michuano mbalimbali ya kimichezo ambayo Misri inaishirikia. 


Katika muktadha huo, Waziri wa vijana na Michezo amesisitiza ushirikiano na Mamlaka ya Michezo ya Kijeshi katika kutoa msaada na utunzaji wote kwa washiriki bora wa wanachama wa shule za michezo za kijeshi, akisifu kujali kwa mamlaka ya michezo ya kijeshi katika jukumu la michezo, elimu ya mwili na mashindano ya michezo, pamoja na jukumu maarufu la mamlaka katika kuandaa mabingwa wanaofanya mafanikio kwa Misri katika vikao mbalimbali vya kimataifa.


Comments