Programu ya "Mwananchi wa Ulimwengu " yaonyesha jinsi ya kuepuksha habari bandia

Kipindi cha tatu cha program ya "Mwananchi wa Ulimwengu " ilizindua mtandaoni, ikitoa mwangaza juu ya hali ya kisasa ya vyombo vya habari barani Afrika na Asia, jinsi ya kuzuia habari zisizo sahihi na habari bandia, changamoto na masuluhisho yake.

Kipindi cha tatu cha programu hiyo kimekaribisha "Shawn Asembo", mtangazaji wa Programu za kimichezo za runinga na Mtoaji, na "Jules Guiyang", mtangazaji wa Mtandao wa Televisheni ya Watu wa Ufilipino, PTV-4, mjumbe wa Baraza la Ushauri la Vijana la Umoja wa Mataifa, kujadiliana mabadiliko ya kisasa katika uwanja wa Vyombo vya habari.

Shawn alisema akiwa mwanamke, changamoto kubwa zaidi katika kazi yake ilikuwa kutilia shaka kutoka wanaume kwa uwezo wake kama mtangazaji wa kimichezo wa Televisheni, lakini alijiwekea mwenyewe na akapata maarifa ya kuwa mwandishi mwenye mafanikio na mtangazaji wa michezo.

Wakati ambapo huko Ufilipino na nchi tofauti za Asia, Jules alielezea kwamba kumekuwa na uwakilishi sawa wa wanawake na wanaume katika sekta ya vyombo vya habari mnamo miaka michache iliyopita.

Shawn alisisitiza kwamba vyombo vya habari vinapaswa kuzingatia kile vinavyokichapisha na kupata habari sahihi na kuidhibiti kabla ya kuchapisha kwa Hadhira.

Jules alishauri umma kuwa na busara wakati wa kushughulika na habari kwenye Mawasiliano ya kijamii, na kuhakikisha uhalisi wake kabla ya kushiriki, kuupongeza au kutoa maoni kwake kupitia kuangalia chanzo cha habari hiyo.

Mwishoni mwa mkutano , Shawn alitaja ziara yake nchini Misri mwaka jana na aliusifu Uandaaji wa Misri kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, pia alieleza furaha yake kwa kuitembelea Misri na Kuhudhuria Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mkutano huo ulitolewa mtandaoni kupitia kurasa za Wizara ya Vijana na Michezo kwenye Mawasiliano ya kijamii, ukiandaliwa na Ofisi ya Vijana ya Kiafrika na Idara kuu ya mipango ya kiutamaduni na hiari kwenye Wizara .

Imetajwa kuwa orodha ya wageni ya Programu ya Mwananchi wa Ulimwengu ni pamoja na watoa maamuzi na viongozi vijana kutoka nchi tofauti za ulimwengu na katika nyanja tofauti , kwa lengo la kueneza ujumbe chanya kwa vijana wa ulimwengu kuunda kiunganishi kati ya vijana na watoa maamuzi.

Comments