Bingwa wa Dunia wa Skwashi Raneem El-Walily aacha mchezo kwa maneno yenye hisia

Raneem El-Walily , mwenye miaka 31, aliamua kustaafu  mchezo ya Skwashi kama mchezaji baada ya safari ndefu ambapo alipata mafanikio makubwa.


Bingwa huyo mmisri aliandika barua ndefu kwa mashabiki wake wote, wapenzi na marafiki, kama ifuatavyo:


Familia yangu mpendwa wa Skwashi, mnamo miaka ya hivi karibuni iliyopita, pengine nimeshafikiria maneno hayo akilini mwangu mara elfu, Skwashi huo ulikuwa maisha yangu kwa miaka 25, na sasa wakati umeshafika kuanza ukurasa mpya.


Ilikuwa safari nzuri, na sikuwahi kufikiria itanichukua mbali kama ilivyo. Nilikuwa na bahati nzuri kwamba kwa miaka kadhaa, nilikutana na vizazi tele , pamoja na wakubwa huko Misri na ulimwengu, nilijifunza kutoka kwao mambo mengi sana , na ninafurahi kuwa nilishiriki mnamo kipindi chema zaidi cha vipindi vyema vya mchezo.


Kwa mara ya mwisho samahani, nitazidi maneno yangu kwa sababu uandishi daima ni njia ya kujieleza iliyokuwa karibu na moyo wangu.


Mtu yeyote miongoni mwenu ananijua vizuri, anajua kwamba naangalia  mahusiano yangu pamoja na watu walio karibu nami, kwa hivyo msishangae kutoka barua hiyo, naiandika hasa kuwashukuru watu wote waliokuwa karibu nami na kunisaidia kuendelea na safari kwa  neno au hata tabasamu.


 Mwanzoni, bila shaka nitaanza na jambo kubwa na muhimu zaidi  maishani mwangu, wazee wangu"Baba na Mama" , ambao bila shaka wana fadhila kubwa sana kwa yote niliyoyapata maishani mwangu.


Asante kwa kujitolea kwenu na upendo wenu.


Pili, Tamim ndugu yangu, ambaye daima sina la kusema kwa kumsifu.

 Je! Yeye ni Meneja wangu wa biashara, kocha, rafiki, au kakangu?


Ukweli ni kwamba yeye ni hayo yote pamoja.


Asante, kwani wewe daima ni msaada wangu.


Kwa familia yangu kubwa na nzuri, nikisema mengi sitawapa haki zao . Mlikuwa pamoja nami katika kila hatua ya njia na siku zote nitakuwa na shukurani kubwa kwenu. 


Na sasa, tumeshafikia  sehemu ngumu zaidi.


Miongoni mwa Neema za Mwenyezi Mungu kwangu, ni nilifanya mazoezi na makocha wengi, kila mmoja alikuwa na vipawa kwa njia yake maalum, na kila mmoja alinifundisha mengi na kunifaidi mengi kutokana na uzoefu wake kwenye mchezo huo na upendo wake kwa maisha. Ikiwa ningekuwa  na nafasi ningemtaja  kila mmoja kwa jina. Na,  Mwenyezi Mungu akipenda, nitafanya hivyo hivi karibuni.


Niruhuse sasa nawashukuru timu ninayoimaliza  kazi yangu pamoja nayo, kwa sababu nilitumia zaidi ya miaka 10 pamoja nayo.


Daima naona kwamba Sehemu muhimu zaidi kati ya Kocha na wachezaji wake ni Ufahamu,nami naweza kusema kuwa pamoja na timu hiyo nimeweza kupata Sehemu ya juu zaidi ya Uwinao n Ufahamu.


Mnamo 2010, nilianza mazoezi ya Skwashi  pamoja na Kocha Haitham Efat, na tangu wakati huo, ana jukumu la kukuza utendaji wangu uwanjani.


Kupitia talanta yake na mtazamo wa mbele, nimefanikiwa kufikia kiwango bora zaidi ya mara moja.


Tukinazungumzia uzima wa mwili, basi Kocha Ahmed Farg Allah yeye ndiye aliyenisimamia  mguu wangu kwenye uwanja kutoka 2009. Kwa miaka mingi, tumeweza kuendelea na kujiboresha wenyewe na kukua pamoja.


Sitasahau kamwe juhudi zake na uchovu wake pamoja nami.


Ingawa nina hakika kuwa wawili wataendelea kuwa sehemu kubwa ya maisha yangu,  lakini jambo muhimu zaidi nitakalolikosa katika suala hilo ni mawasiliano yetu na mikutano ya kila siku.


Mtu anayefuata ni mtu muhimu sana kwangu, na niliwasiliana naye kwa bahati baada ya jeraha langu kwenye Mashindano ya Dunia kwenye Wadi Degla mnamo 2014.


Daktari Mohamed Amin, kwangu, yeye ndiye mtu niliyemwamini zaidi na talanta yake katika safari ya matibabu ya mwili.


Napenda pia, kumshukuru Daktari Hany Wahba, Daktari wa lishe ya michezo, aliyenifaidika  sana mnamo miaka miwili iliyopita.


Pia, Bi Hala Mitwalli, mtaalam wa raha ya mwili, ambaye kila wakati alikuwa akinipa nguvu chanya.


Siwezi kusahau jukumu la marafiki zangu, licha ya kuzembea kutoka kwangu kwa sababu ya wakati wangu mdogo, lakini kila mara walikuwa wakisimama pamoja nami kwenye safari hii, katika uzuri na hata uchungu wake.


Wadi Degla, ambapo nimepata raha yangu mnamo miaka saba iliyopita, na pamoja nao nimeweza kufanikiwa  mafanikio yangu muhimu zaidi.


Familia ya Wadi Degla yote nitaikosea na wachezaji wake, wazazi, usimamizi na makocha. Ilikuwa heshima kwangu kuwakilisha timu hii kubwa.  Napenda kumshukuru sana Karim Darwish kwa juhudi zake, na kwa kunipa nafasi kama hii. 


Ilikuwa heshima kwangu wakati wa uzoefu huo,  kukutana na Bwana Hussein Abaza.


Kwa wenzangu wote kwenye mchezo huo, hasa Wamisri, na hasa pia Wasichana, ilikuwa heshima kubwa kwangu kushindana na nyinyi wakati wote wa safari. Asanteni kwa kumbukumbu nzuri zote. Nitawakosea sana.


Mashabiki na wapenzi wakubwa wa Skwashi na hasa wapenzi wamisri,  nyinyi ni ndio msingi wa mchezo huo na msingi wa mafanikio yetu. Asanteni kwa msaada wenu usio na mwisho.


Mwishoni, asante, Mume wangu mpendwa. Ni kweli kwamba ni baraka kubwa sana ikiwa tuna uwezo na fursa ya kuendelea katika njia hii pamoja, na kushirikiana. Walakini, Neema halisi ni kwamba ulikuwa na subira sana, ulinipa nafasi, na nilifikia kwa hatua hii kwa wakati ambayo ingeweza kunifariji bila mashinikizo yoyote.


Na ninatamani kufanikiwa kumaliza safari hii kwa muda mrefu iwezekanavyo.


Sijapanga chochote mnamo kipindi kijacho, lakini inaonekana kuwa nitaangalia  familia yangu ndogo, na natamani kuwa nitaweza kukabiliana na changamoto za maisha zijazo.


Labda ninaaga  mashindano ya Skwashi, lakini siagi  kumbukumbu zake, urafiki, mahusiano, na siku zake zote nzuri, pamoja na leo. "

Comments