Ahmed Ahmed, Rais wa Shirikisho la kiafrika la Soka (CAF), alimshukuru Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa kukubali kwake kuendelea kwa makao makuu ya CAF mjini Kairo.
Jumanne, Rais wa Shirikisho la kiafrika, wakati wa mkutano wa kamati ya kiutendaji kwa shirkisho kupitia mikutano ya Video alisema: "Ninamshukuru na namheshimu Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamuhuri ya Kiarabu ya Misri , na serikali ya kimisri, kwa kusaini makubaliano ya makao makuu, yatakayoruhusu kuwepo kwa makao makuu ya CAF mjini Kairo kwa miaka kumi ijayo".
Aliongeza, "Kulingana na makubaliano mapya, wafanyikazi wa Shirikisho la Soka la kiafrika watapata faida nyingi, maarufu zaidi ni kinga iliyopewa misheni ya kidiplomasia inayoendesha kwenye eneo la Jamhuri ya Kiarabu ya Misri".
Comments