Waziri wa Michezo ajadili maandalizi ya kukaribisha Mashindano ya Ulimwengu kwa Sarakasi ya kiufundi
- 2020-07-04 19:51:56
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na Dokta Ihab Amin, Rais wa Shirikisho la Misri la Sarakasi , kujadili maandalizi ya kukaribisha Misri kwa Mashindano ya Ulimwengu ya Sarakasi ya kiufundi mnamo Juni 2021.
Mkutano huo ulionyesha maandalizi yote na hatua zilizochukuliwa na Shirikisho la Misri la Sarakasi kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa kwa mchezo kuhusu kukaribisha Misri kwa Mashindano ya Ulimwengu , ili kuyatoa katika picha bora zaidi.
Mkutano huo ulijadili pia kile kilichokamilishwa kwa suala la kupeana vifaa vya kisasa kwa shirikisho la Sarakasi kwa msaada wa Wizara ya Vijana na Michezo ili kuweka Shirikisho la Misri kwenye ramani ya Ulimwengu kukaribisha mashindano ya kimataifa ya Sarakasi.
Wakati wa mkutano huo, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza utunzaji wa serikali ya kimisiri , inayoongozwa na Waziri Mkuu Dokta Mostafa Madbouly, kutoa misaada yote kwa mfumo wa michezo wa Misri ili kuiweze kukaribisha mashindano ya kimataifa ili kuiweka Misri daima katika mstari wa mbele katika uwanja wa michezo wa kimataifa, aliashiria maandalizi ya kukaribisha wa Kombe la mkono Januari 2021 Inafanywa kwa ufanisi kwa msaada wa Wizara na kufuata kwake, kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki ya Misri na mashirika yote ya michezo, ili kusisitiza utayari wa mahitaji yote yanayofanikiwa kukaribisha Misri kwa Mashindano tofauti ya kimataifa na ya Kiafrika.
Waziri alionyesha umuhimu wa kuendelea michezo ya Sarakasi na kufanya bidii kwa kuieneza zaidi kwa kushirikiana na Shirikisho la mchezo huo mnamo kipindi kijacho.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Sarakasi alisifu juhudi za Waziri wa Vijana na Michezo na dhamira yake ya kuendeleza mfumo wa michezo na kuunga mkono mashirika ya michezo, akionesha umuhimu wa vifaa vya kisasa ambavyo wizara hiyo ilitunza kuipatia kwa shirikisho la Sarakasi, vinavyozingatia sababu kubwa inayoongezwa kwa viungo vya Misri wakati wa kuomba kukaribisha mashindano ya kimataifa kwa Sarakasi .
Comments