Sobhy asimama Mkutano wa Ofisi ya kiutendaji kwa Baraza la mawaziri waarabu wa Michezo kupitia mikutano ya video
- 2020-07-08 23:14:10
Alhamisi asubuhi, Mkutano wa Ofisi ya kiutendaj kwa Baraza la mawaziri waarabu wa Vijana na Michezo ulianza kikao chake cha 40 kwa sanduku la Kiarabu kwa shughuli za vijana na Kiarabu , na pia kikao cha 65 cha Ofisi ya kiutendaji ya Baraza la mawaziri Waarabu wa Vijana na Michezo , kilichoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na mwenyekiti wa Ofisi ya kiutendaji kwa Mawaziri Waarabu wa Vijana na Michezo , kupitia mikutano ya video , kwa mahudhurio ya Mawaziri Waarabu wa vijana na michezo, wanachama wa Ofisi ya kiutendaji.
Sobhy alianza hotuba yake kwa kuwakaribisha Waziri wa Vijana na Michezo wa Jamhuri ya Tunisia Mheshimiwa Ahmed Kaaloul, na Waziri wa Vijana na Michezo wa Jamuhuri ya Iraqi Waziri Mheshimiwa Adnan Darjal waliojiunga na uanachama wa Ofisi ya kiutendaji, kufuatilia wote wawili Profesa Sania bin Al-Sheikh Waziri wa zamani wa Vijana na Michezo wa Jamhuri ya Tunisia, na Waziri wa Vijana na Michezo wa Jamhuri ya Iraq Ahmed Riyadh Abo Taleb Al-Ubaidi, akiwatakeni kila la kheri.
Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuendeleza shughuli na programu zinazotekelezwa na ambazo zimesaidia sana katika kubadilishana uzoefu na ujumuishaji wa maadili na kanuni kati ya vijana waarabu, akisisitiza umuhimu wa kutoa fursa kwa idadi kubwa kwa vijana kushiriki katika shughuli, matukio na programu ambazo kwa sasa zinatekelezwa kupitia mikutano ya video , au baadaye baada ya kumalizika kwa mzozo wa Corona, na akiongeza kuwa wote wanapaswa kuwasaidia vijana katika nchi zote na kuwahimiza kuwa na ubunifu na uvumbuzi katika shughuli wanazoshiriki, na kueneza uzoefu wao kati ya vijana waarabu wanaoshiriki katika shughuli hizo, ambayo husaidia vijana wote wanaoshiriki ili kujihusisha zaidi.
Mkutano huo ulijadili kuanzishwa kwa mkutano wa 17 wa vijana wa miji mikuu ya Kiarabu katika Ufalme wa Hashemite wa Jordan, ukipendekeza kuanzisha mkutano wa kuunga mkono kwa Al-Quds tukufu, Programu ya Uwezeshaji wa Vijana waarabu katika Ufalme wa Saudi Arabia, saluni ya vijana waarabu kutoka mbali , "Mtazamo wa vijana waarabu baada ya Corona ", mpango wa uigaji Bunge la Vijana la Kiarabu, kusisitizia Kutekelezea maagizo yaliyotolewa na Mkutano wa Kimataifa wa mpango wa Vijana kwa kutumia teknolojia ya habari na uhusiano wake na kukandamiza ugaidi, uliyofanyika nchini Misri Januari 2020.
Haifa Abu Ghazaleh, Katibu Mkuu Msaidizi wa Taasisi ya Kiarabu na Mwenyekiti wa Sekta ya Masuala ya kijamii, alifikisha salamu za Ahmed Abu ElGhet, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiarabu kwa mawaziri, akitamani kwamba mkutano ujao uatawajumuishwa baada ya kumalizika kwa mgogoro wa virusi vya Corona.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta Amr Al-Haddad, Msaidizi wa waziri wa Vijana na Michezo kwa Maendeleo ya Michezo, na Bwana Abdel Moneim Al-Shaari, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana na Michezo kwenye Ligi ya Nchi za Kiarabu.
Comments