Waziri wa Michezo atangaza maelezo ya mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako"

Sobhy .. Wizara inatoa Nafasi ya kupata baiskeli kwa njia ya kielektroniki kwa bei nafuu katika mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako"

Na anasisitiza : Mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako" unachangia kueneza mazoezi ya michezo na kuhifadhi mazingira ... na mpango huo unazinduliwa kwa kupatikana baiskeli elfu.

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alitangaza kuwa mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako" unaoshikiliwa na Wizara, utaanza kutosheleza baiskeli 1,000 kwa bei nafuu kwa raia, na tunakusudia kuongeza idadi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya kiarabu kwa Viwanda mnamo mwaka wa kwanza wa mpango huo, sambamba na maagizo ya uongozi wa kisiasa kwa kupanua msingi wa mazoezi ya Michezo, ili kuchangia kueneza michezo na kuifanya iwe mtindo wa maisha kama moja ya mihimili mikuu ya mkakati wa shughuli za Wizara."

Hayo yalikuja wakati wa shughuli za mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika na Wizara ya Vijana na Michezo, leo, Jumatano, kwenye Kituo cha Elimu ya kiraia huko Al Gazira, kwa mahudhurio ya Jenerali Abd El Moneim El-Terras, Mkuu wa Taasisi ya kiarabu kwa Viwanda, na Tarek Fayed, Mkuu wa Benki ya Kairo.

Katika kauli yake, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba Mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako" unalenga kuwahamasisha raia kufanya mazoezi ya michezo, na unategemea mihimili miwili mikuu: wa kwanza ni kuboresha Uzima wa mwili na afya kwa raia kupitia matumizi ya "Baiskeli", na mhimili wa pili unazingatia "Baiskeli" ni njia ya kusafiri inayoambatana na mazingira.

Dokta Ashraf Sobhy alieleza kuwa bei ya Baiskeli iliyotangazwa ni rahisi , mwafaka na inasaidiwa na Wizara, pamoja na njia rahisi katika malipo, vijana na wananchi wanaotaka kununua Baiskeli wanaweza kuingia kwenye lango la kielektroniki la Wizara, kujaza taarifa zinazotakiwa na kuchagua aina ya baiskeli inayohitajika, akitoa shukrani kwa washiriki wote kwa kufanikiwa katika kutekeleza mpango huo, na kutoa misaada yote kwake, kufikia malengo yaliyotarajiwa kutoka kwake katika ngazi tofauti.

Kwa upande wake, Jenerali Abd El Moneim El-Terras alielezea kuwa baiskeli zilizotangazwa ndani ya mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako" ni kutengeneza kamili kwa kimisri, na zinatolewa kwa vijana na raia, na kuwahamisisha kuzinunua kwa kuzingatia mabadiliko ya ujenzi yanayoshuhudiwa nchini katika kiwango cha barabara na miji mipya ambayo wakati wa kuipanga huzingatia mielekeo na njia hasa kwa Baiskeli.

Mkuu wa Taasisi ya kiarabu kwa Viwanda alielezea shukrani zake za dhati kwa Waziri wa Vijana na Michezo kwa ushirikiano mzuri pamoja na Taasisi ya kiarabu kwa Viwanda katika miradi kadhaa ya maendeleo, pia mchango wake katika kuendeleza mfumo wa michezo, programu, miradi na mipango iliyotolewa kwa ajili ya vijana katika nyanja tofauti.

Wakati ambapo Bwana Tarek Fayed, Mkuu wa Bodi ya idara ya Benki ya Kairo, alithibitisha ushiriki wa benki katika mpango huo , kwa kuzingatia mchango wa kijamii wa benki, na kuuzingatia mpango huo ni mradi wa kitaifa unaohitaji mshikamano wa wote ili kufanikiwa, akitamani kufikia baiskeli milioni moja mnamo mwaka wa kwanza wa mpango huo , kuzingatia faida zake chanya kwa afya ya raia, Na urahisi wa kuhamia.

Wizara ya Vijana na Michezo inatoa nafasi ya kununua Baiskeli ndani ya mpango wa "Baiskeli yako ni Afya yako" kwenye mitandao kupitia lango la kielektroniki la Wizara kupitia linki ifuatayo:.

https://www.emys.gov.eg/details/11497

Comments