Balozi wa Misri alitoa barua ya pongezi kutoka kwa Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri kwa Waziri mpya wa Mambo ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni huko Brundi

 Dokta Abeer Bassiouni Radwan, Balozi wa Misri nchini Burundi, alitoa barua ya pongezi iliyotumwa na Waziri wa Mambo ya nje, Sameh Shoukry kwa mwenzake wa Burundi, "Albert Shingro", Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Maendeleo nchini Burundi, kwa mnasaba wa kushikilia kwake kwa majukumu  katika serikali mpya ya Burundi.


Pia balozi wa Misri  alitoa barua ya pongezi kutoka kwa Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri, Dokta Ashraf Sobhy   kwa Waziri mpya  wa Mambo ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni " Ezechiel Nibigira" wakati akimpokea katika makao makuu ya  Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


 Balozi wa Misri alijadili na maafisa wa Burundi  kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa nchi mbili za  Misri na Burundi katika nyanja zote tofauti, kwa kuzingatia viunganishi vya kihistoria na mahusiano yenye kina yanayounganisha nchi hizo mbili.


Comments