Waziri wa Michezo ajadili maandalizi ya Misri ili kukaribisha michuano ya Dunia ya Wavulana katika Silaha 2021
- 2020-07-28 21:57:34
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Jumatatu jioni, alimpokea Dokta Adel-Moneim El-Husseini, Mwenyekiti wa Shirikisho la Silaha la kimsiri, akiambatana na wanachama wa baraza la uongozi la Shirikisho.
Wakati wa mkutano huo, Waziri wa Michezo alitangaza kwamba Misri itakaribisha Mashindano ya Dunia ya silaha katikati ya mwaka ujao 2021.
Sobhy alisisitiza wakati wa mkutano kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ina nia ya kutoa utaalam wake wote na kutoa fedha, kiutawala na vifaa katika kuandaa tukio hilo la ulimwengu ili lionekane kwenye sura yenye heshima inayoonyesha msimamo wa Misri kwa kiwango cha kimataifa na uwezo wake wa uandaaji ulimwenguni, hasa kuhusu kukaribisha hafla kubwa zaidi za kimataifa za kimichezo.
Inatarajiwa kwamba wachezaji 1,600 na watawala na mafundi 500 wanaowakilisha nchi 100 watashiriki kwenye mashindano hayo, na mashindano hayo yatafanyika mnamo kipindi cha tarehe 4 hadi 11 Aprili, mwaka wa 2021.
Inatajwa kwamba mara ya mwisho Misri kukaribisha michuano ilikuwa mnamo mwaka 1962.
Kwa upande wake, Abd El-Moneim El-Hussini alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa juhudi zake katika uwanja wa michezo, hasa Shirikisho la Silaha la Kimisri.
Comments