Ashraf Sobhy anapongeza Hana Gouda baada ya kumchagua toka Shirikisho la kimataifa kwa Tenisi ya Meza ili kuwakilisha Misri na Bara la Afrika.

Dokta Ashraf Sobhy "Waziri wa vijana na michezo "alipongeza mchezaji mmisri Hana Gouda  baada ya kumchagua toka Shirikisho la kimataifa kwa Tenisi ya Meza akiwakilisha kwa Misri na Afrika katika kambi la AlAml la kimataifa, na michuano ya dunia chini ya miaka 12 itakayofanyika kwenye Oman mnamo kipindi cha 25 hadi 31 Julai ujao.

 

Sobhy alieleza furaha yake kwa uchaguzi wa Shirikisho la kimataifa kwa Tenisi ya Meza kwa Hana Gouda ili kuwakilisha Misri na Afrika, akiongeza kwamba Wizara inaangalia wachezaji wote khasa wenye vipaji na mustakbali nzuri, akimwambia Hana kufanya mazoezi mengi kwa ajili ya kuongeza kiwango chake cha kisanaa, akiongeza kwamna Hana ni kipaji kizuri sana na Wizara inafanya kazi ya kutosheleza njia zote za kumsaidia na kurahisisha vikwazo vyote vinavyopo mbele ya ndoto yake kwa kuhakikisha Medali ya kiolompiki.

 Hana Gouda alishukuru Dokta Ashraf Sobhy, na alieleza furaha yake kwa Heshima hii akiongeza kwamba pia yeye anafurahi kwa kuwakilisha Misri baada uchaguzi wa Shirikisho la kimataifa kwa Tenisi ya Meza kwake, akisistiza kwamba atajitahidi  daimaili kuboresha kiwango chake cha kisanaa kupitia kupanga kwa njia ya kudumu kwa makambi na michuano ya ndani na nje ili kufikia ndoto yake ya kimichezo ya kimataifa na kiolompiki, pia ili kupepea jina la Misri juu kwenye sherehe za kimataifa, na Hana alieleza kwamba anatarajia kupata Medali katika Olempiad 2024.

 

Inayolazimisha kutajwa ni kwamba binti mwenye miaka 11 aliweza kupata idadi kubwa toka Medali katika michuano tofauti, miongoni mwao ni Medali ya kidhahabu katika michuano ya Algeria ya kimataifa mwaka wa 2016, Medali ya kifedha katika michuano ya Swid 2017,na ya kidhahabu ya michuano ya Tunisia na michuano ya kiafrika 2018,pamoja na yeye ni mchezaji wa kwanza wa umri wake chini ya miaka 12.

 

Heshima hii ilihudhuria na Bwana Muhamed ElMoataz Ashour "Rais wa Shirikisho la kimisri kwa Tenisi ya Meza", na Dokta Radwa Azab "Mama wa mchezaji".

Comments