Waziri wa Michezo ahudhuria mechi ya Al-Ahly na Enppi baada ya kuanza tena kwa Ligi Kuu
- 2020-08-11 12:59:00
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, jioni ya leo, Jumapili, anashuhudia mechi ya Al-Ahly na Enppi katika mashindano ya Ligi Kuu ya Kimisri katika awamu iliyoahirishwa kati ya klabu ya Al-Ahly na klabu Enppi kutoka wiki ya kumi na tano ya Mashindano ya Ligi ya Soka ya Kimisri , baada kurudi tena kwa Ligi ya Misri kutokana na kusimamishwa kwa sababu ya kuenea kwa virusi vya Corona .
Sobhy alihakikishia hatua zote za tahadhari zilizochukuliwa kabla ya kuanza kwa mechi ya Al-Ahly na Enppi katika suala la kupima joto, kusafisha uwanja na maeneo yote ambayo wachezaji wanapopatikana, na kuwepo kwa msimamizi wa matibabu; Kufuatilia utekelezaji wa taratibu na mahitaji yote ya kiafya.
Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza ufuatiliaji na uratibu na mashirikisho ya michezo kuhusu kurudi pole pole kwa mashindano hayo kwa mujibu wa mahitaji ya tahadhari na hatua za utekelezaji ambazo tayari zimetangazwa, akiashiria kuwa usalama na afya ya wachezaji huwekwa na Wizara na mashirikisho mbele ya vipaumbele, na kuna ufuatiliaji kwa mabadiliko yote, na kuchukua hatua za haraka ikiwa kuna mgonjwa wa virusi vya Corona.
Ikumbukwe kuwa Dokta Ashraf Sobhy alishuhudia mechi ya Zamalek na Al-Masry iliyofanyika jioni ya Alhamisi kwenye Uwanja wa Borg Al Arab huko Aleskandaria katika mechi ya kwanza wa ligi baada ya kuanza tena kutoka kwa sababu ya kuenea kwa virusi vya Corona .
Mashindano ya Ligi kuu ya Mpira wa Miguu ya Kimisri yanarudi kulingana na hatua na mahitaji ya tahadhari, na kulingana na mwongozo uliotolewa na Wizara ya Vijana na Michezo kuhusu kurudishwa kwa shughuli za michezo katika mashirikisho mbalimbali ya michezo, na baada ya kukamilika kwa vipimo vyote vya matibabu kwa wachezaji na vifaa vya kiufundi na vya kiutawala kuhakikisha usalama wao na kuhifadhi afya zao.
Comments