Waziri wa vijana na michezo atafuta pamoja na wasaidizi wake kuanza tena shughuli za Siku ya Vijana ya Kimataifa
- 2020-08-11 13:01:10
Dokta Ashraf Sobhy waziri wa vijana na michezo alijadili maandalizi na Mipangilio ya shughuli za Siku ya Vijana ya Kimataifa na inayoamuliwa kufanyikwa mnamo Agosti 12 hii , kwa kichwa cha " Ujihusishaji wa vijana kwa ajili ya ushiriki wa ulimwengu " , pamoja na wasaidizi wa waziri na viongozi wa wizara .
Na waziri wa vijana na michezo alisema kwamba uwekezaji katika kipengele cha binadamu na kuandaa mazingira yanayomunga mkono ni Sehemu muhimu ya maoni ya wizara , akiashiria umuhimu wa kufanya kazi kwa kuwaandaa vijana kupitia kuendeleza ujuzi wao wa maisha , ujuzi wa kufanya kazi na kuandaa miradi midogo ambapo Inakidhi mahitaji ya soko la ajira , hasa katika sekta binafsi .
Na kila mwaka ulimwengu unasherehekea Agosti 12 na hivyo ni kwa umuhimu wa Ushawishi wa vijana katika jamii zao na majukumu yao bora katika maendeleo , na nchi inayowakilishwa katika wizara ya vijana na michezo na mamlaka ya umoja wa mataifa nchini Misri ilizoea kusherehekea siku hii kama uthibitisho wa msaada wao ili kuendeleza ujuzi wa vijana nchini Misri na kusisitiza jukumu lao la kushughulikia na janga la Corona .
Waziri wa michezo alijadili kuanza tena shughuli na maandalizi yanayohusu mradi wa kitaifa wa vipaji , bingwa wa olimpiki na awamu na hatua za kuwachagua Watu wenye talanta katika michezo tofauti kupitia Kamati za kisayansi na za kifanii zinazohusiana na hivyo .
Na waziri wa vijana alijadili maelezo ya mpango wa " Baiskeli yako ni Afya yako " akisisitiza Mwendelezo wa mpango kupitia mkutano mnamo kipindi kijacho na kupanuka kijiografia kupitia ufunguzi wa vituo vya usambazaji katika mikoa mbalimbali .
Akiongezea kwamba njia pekee ambayo kupitia yake Baiskeli zinauzwa katika mpango ni kupitia kujiandikisha katika lango la kielektroniki la wizara pamoja na kupata njia ya Uhifadhi endelevu kutokana na maoni ya uongozi wa kisiasa na maagizo ya heshima yake kufanya kazi kuhusu usambazaji wa Mazoezi ya michezo ili kuhifadhi afya ya umma na viwango vya usawa wa mwili wa wananchi wote hasa vijana kupitia kucheza Baiskeli.
Comments