Waziri wa michezo ajadili mawazo na mipango mipya katika "semina ya vijana " ya kila wiki
- 2020-08-12 22:26:10
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo alijadili mawazo na miradi mipya inayotolewa na wafanyakazi wa Wizara ya vijana na michezo kupitia " semina ya vijana " inayofanyikwa kila wiki kwa majadiliano kadhaa.
Vijana wa Wizara walieleza kundi la mipango na mipango muhimu zaidi ni mpango wa kongamano la kisayansi la kudumu la mabalozi wa vijana wa Misri , kuendeleza jamii na uenezi wa Amani , mpango wa kituo cha kitaifa cha Uwezeshaji wa vijana na wachipukizi, mpango wa kongamano la wafanyakazi katika Wizara ya vijana na michezo na idara ya ubora katika mamlaka zinazohusu Wizara na pia utekelezaji wa kozi kadhaa za mafunzo zinazoenda sambamba na mahitaji mapya ya kiteknolojia.
Katika muktadha huo huo , Sobhy aliamuru kuagalia mipango yote inayotolewa na vijana wa Wizara pamoja na idara husika ili kufanya kinachotakiwa , pamoja na kuongeza njia za kuifaidika kutoka kwake kama iwezekanavyo na kuiweka uhalisini ili itekelezwe.
Na Waziri wa vijana na michezo alisisitiza kwamba jukumu la semina hii ni kujadili mawazo na maudhui mpya zinazuhusu kuendeleza kazi katika taasisi za wizara na mamlaka za vijana na za michezo , kuendeleza na kuunda upya miradi inayotolewa na wizara kwa sekta tofauti za watoto, vijana na michezo nchini Misri, inayokuja miongoni mwa maoni yanayowekwa na Rais wa nchi Abd El-Fatah El-Sisi katika kupitishwa mawazo na maoni ya vijana wamisri na ambayo yakawa ishara na alama za nchi ya Misri na alama muhimu zaidi ni mikutano ya vijana na inayofanyika chini ya usimamizi wa uongozi wa kisiasa.
Comments