"Sobhy ashuhudia kutia saini kwa makubaliano ya ushirikiano pamoja na kampuni ya nyasi ya kiwanda ya kijerumani "
- 2020-08-12 22:28:18
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo , Jumatatu, ameshuhudia shughuli za kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara ya vijana na michezo na kampuni ya nyasi ya kiwanda ya kijerumani kuhusu kuendeleza utendaji wa kiwanda cha nyasi kinachohusishwa na kampuni ya kimisri ya kutengeneza vifaa na vyombo vya michezo ( CAPTEX) nayo ni kampuni ya pamoja ya hisa ya kimisri inayohusisha na sanduku la ufadhilii la Al Ahly la kutunza wachipukizi , vijana na michezo linalohusisha na Wizara ya vijana na michezo , Wizara ya nchi kwa uzalishaji wa kijeshi na kampuni ya Makasa ya michezo .
Waziri wa vijana na michezo
alisisitiza kuwa kiwanda cha Nyasi kinazingatiwa kuwa mojawapo ya miradi ya michezo muhimu zaidi kitakachokuwa na jukumu linaonekana wazi kwenye uchumi wa kimisri katika kipindi kijacho , akiashiria utiliaji mkazo wa wahusika wa mradi kwa kuendeleza mifumo ya kazi na kusahihisha njia ili kutimiza malengo ya mradi huo yanayotarajiwa , akisisitiza kuwa ndio ni wa kipekee nchini Misri , eneo la Mashariki ya kati na Afrika unaotegemea malighafi ya hali ya juu ya kijerumani kwa bei za ushindani kupitia mifumo ya uzalishaji mpya na ya hali ya juu kwa ushirikiano na kuambatana na upande wa Ujerumani .
Waziri wa vijana na michezo alisema kwamba kwa mujibu wa makubaliano hayo, bei ya bidhaa ya mwisho itapunguzwa , kufikia bei ya ushindani , kupata malighafi ya ushindani inayoidhinishwa na mamlaka rasmi na kwa ubora mkubwa wa Ujerumani , uwezo wa kampuni wa kufungua masoko mapya barani Afrika na mashariki ya kati na kampuni iwe kama msingi wa mkusanyiko mkubwa wa viwanda vya michezo utakaobadilishwa baadaye kwa mji maalum wa viwanda vya michezo .
Aliongeza kuwa chombo cha usimamizi cha kiwanda kimesharekebishwa ili kuimarisha mazingira ya kazi , kuongeza uwezo wa uzalishaji kutoka mita 500 hadi mita 7500 kwa siku ya kiwanda cha Nyasi bandia na kuzidisha mauzo ya kiwanda ili yapite zaidi ya milioni mia wakati miezi sita iliyopita inayotarajiwa kuongezeka hadi mita za mraba milioni 2.1 kila mwaka .
Ikumbukwe kuwa wazo la kuanzisha mradi huo lilikuwa na makusudi ya kufanya maendeleo makubwa kwa viwanda vya bidhaa na vifaa vya michezo kama Nyasi bandia na vifaa mbalimbali vya michezo vinavyohitajika na soko la kimisri , kiarabu na kiafrika, lililoanzishwa kwa ajili ya kusambaza Nyasi bandia kwa viwanja vya michezo kwa vigezo vya Shirikisho la kimataifa la Soka "FIFA" lililoanza shughuli zake 2019 .
Na wakati wa kuhitimisha kauli yake , Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo aliashiria kuwa umuhimu wa maendeleo haya yanakuja kwa kuzingatia mwenendo wa Wizara ili kuimarisha mchango wa michezo ya kimisri na jukumu lake kwenye uchumi wa kimisri ikiwa kupitia kiwango cha uwekezaji unaotolewa na miradi ya michezo na vijana yenye manufaa ya kiuchumi inayotekeleza marupurupu na faida . Uwekezaji huo hutumika tena katika kutekeleza shughuli , miradi na kuendeleza miundombinu ya michezo na vijana katika mikoa mbalimbali ya Jamuhuri.
Comments