Dokta Mohamed Abd El Ati, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, alimpokea Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo; kujadili ushirikiano kati ya wizara hizo mbili na utaratibu wa kuelimisha vijana juu ya umuhimu wa matumizi bora ya maji ili kukabiliana na changamoto za kisasa na za baadaye.
Mkutano huo ulijumuisha kujadili ushirikiano katika kuwekeza mahali na bustani za umwagiliaji kutekeleza shughuli zingine za michezo katika mbuga za (Afla, Nile na Al Manashe) na mbuga zingine zinazohusiana na Wizara.
Wakati wa mkutano huo, Dokta Ad El-Ati alisisitiza hitaji la kuongeza uelewa wa upungufu wa rasilimali za maji nchini Misri, umuhimu wa kuhama kutoka utamaduni wa maji mengi kuelekea kwenye utamaduni wa matumizi bora, na kufafanua nafasi na asili ya shida ya maji huko Misri, na mkakati wa nchi hiyo kwa maji, unaowakilishwa katika mfumo wa kuboresha, kusasisha na kuendeleza rasilimali za maji, na pia kuongeza uhamasishaji na kujenga mazingira yanayowezesha kukutana na changamoto zinazoikabili nchi katika suala la maji, jambo lenye umuhimu zaidi ni uongezeko wa idadi ya watu licha ya utulivu wa sehemu ya maji kwa Misri.
Abd El-Ati alielezea, utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa rasilimali za maji hadi 2037 kwa madhumuni ya kufanikisha "Usalama wa maji kwa wote", kutoa maji yanayotakiwa kwa matumizi yote kupitia njia za kuongeza rasilimali za maji na kusimamia mahitaji ya maji, na pia kupitia hatua za kurekebisha matumizi ya maji kwa rasilimali duni, kwa kuandaa mkakati wa maendeleo endelevu kwa nchi hadi 2030, kwa madhumuni ya kuiweka Misri miongoni mwa nchi 30 za juu ulimwenguni kiuchumi na kijamii ifikapo 2030.
Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alielezea furaha yake na mkutano muhimu huo, unaokuja ndani ya mfumo wa ushirikiano unaoendelea kati ya Wizara za Vijana na Michezo na Umwagiliaji, na unaruhusu uwekezaji wa bustani na mbuga katika utekelezaji wa shughuli zingine za michezo ili kupanua wigo wa mazoezi ya michezo, na kubaini kuwa Wizara ya Vijana inahangaika kufanya michezo iwe njia ya maisha kwa Wamisri wote, katika mfumo wa maoni ya uongozi wa kisiasa.
Comments