Kwa mahudhurio ya mawaziri kadhaa ... Wizara ya Vijana na Michezo yazindua tamasha la kwanza la michezo huko Al-Alamein

Jumatano, Wizara ya Vijana na Michezo itazindua tamasha la kwanza la michezo katika mji mpya wa El Alamein, kama sehemu ya mpango wa Wizara wa kupanua msingi wa mazoezi ya michezo, kukuza na kutoa mwanga kwenye moja ya miradi muhimu ya kiutalii ambayo inatekelezwa ndani ya Misri mnamo kipindi hiki cha kisasa.


Inatarajiwa mawaziri kadhaa watashiriki katika tukio kubwa hilo , pamoja na vijana kadhaa wanaoshiriki katika shughuli za tamasha hilo, linalojumuisha "mbio za Baiskeli, mpira wa wavu wa pwani, mpira wa miguu ya Khomasi ya Pwani , mpira wa kasi ,na (Street work out) ."


Katika suala hilo, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitizia jukumu la Wizara hiyo na mchango wake mkubwa katika kuunga mkono utalii na miradi ya kitaifa inayotekelezwa na serikali kupitia michezo, ambayo imekuwa moja ya sehemu muhimu zaidi ya taifa kamili, na akiashiria kuwa Wizara hiyo inashirikiana kudumu na kuendelea na Wizara zote, taasisi na sekta ; Kufikia uongezeko wa thamani kwa miradi yote ya kitaifa inayotekelezwa kwenye ardhi ya Misri.


Katika muktadha huo huo, pembezoni mwaTamasha la Michezo hufanyika shughuli za uzinduzi wa harakati wa mashindano ya Jamhuri kwa kampuni katika toleo lake la 53 kwa mara ya kwanza kutoka mji wa El Alamein, na wanariadha zaidi ya elfu 15 wanashiriki katika mashindano wakiwakilisha kampuni kadhaa, viwanda, na sekta za serikali na binafsi.

Comments