Mawaziri wa Michezo na Mawasiliano wajadili vifaa vya kiufundi na kiteknolojia kwa Kombe la Dunia la Mpira wa mikono
- 2020-08-19 10:57:45
Dokta Amr Talaat, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, walifanya mkutano kupitia teknolojia ya mkutano wa video ili kujadili maandalizi ya kiteknolojia na vifaa vya kiufundi vinavyohitajika kwa kumbi zilizofunikwa zitakazokaribisha matukio ya Kombe la Dunia la Mpira wa Mikono uliopangwa kufanywa nchini Misri Januari ijayo.
Toleo la 27 la Kombe la Dunia la mikono ni moja wapo ya matukio maarufu zaidi ya michezo ulimwenguni mnamo 2021. Mashindano hayo yatafanyikwa katika viwanja vinne, navyo ni ukumbi uliofunikwa kwenye uwanja wa Kairo, Ukumbi wa mji mpya wa kiutawala , ukumbi wa mji wa 6 Oktoba , na ukumbi wa Jiji la Borg Al Arab.
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza ushirikiano mkubwa na Wizara zote na mamlaka zinazohusika na uratibu nao ili kutoa vifaa na mahitaji muhimu kwa mashindano hayo kwa kuzingatia utafutaji wa utengenezaji wa mashindano hayo na kuipanga katika kiwango bora kinachofaa uwezo wa Misri kwa kukaribisha mashindano makubwa ya kimataifa ya michezo.
Dokta Ashraf Sobhy alisifu michango ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika matukio mbali mbali ya kimataifa uliyofanyika nchini Misri, na utoaji wa zana zote za mawasiliano na teknolojia ya kisasa ndani ya majengo ya michezo yanayoshikilia mashindano hayo kulingana na viwango vinavyohitajika vya kimataifa.
Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dokta Amr Talaat alithibitisha utayari wa Wizara hiyo kutoa msaada muhimu wa kiufundi kuandaa viwanja ambapo mashindano hayo yatafanyika kwa kuwapa vifaa, mahitaji ya kiufundi na huduma muhimu za mawasiliano na teknolojia ya habari na viwango vya kimataifa vya kuzalisha mashindano hayo kwa njia inayolingana na msimamo wa kiteknolojia na Ambayo ni kushuhudia ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mingi ya kitaifa inayolenga kujenga Misri ya dijiti, ikiashiria kwa ushirikiano kati ya Wizara za Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Na wizara ya vijana na Michezo katika nyanja kadhaa, maarufu zaidi ambayo ilikuwa ni utoaji wa mahitaji ya kiteknolojia muhimu ya kukaribisha Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu mwaka jana.
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kwa kushirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo, zimeangalia tena vifaa vyote vya uhandisi kuandaa mitandao ya mawasiliano kwa kumbi mpya ambazo zinajengwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya Shirikisho la Kimataifa, na mahitaji yote ya Shirikisho la Mpira wa Mikono wa Kimataifa na Kamati iandaayo kuhusu vifaa, na mtandao wa interneti na miundombinu ya mawasiliano.
Katika muktadha huu, ilikubaliwa kutoa viwanja hivi na teknolojia za kisasa zaidi za kimataifa, kuandaa vituo vya waandishi wa habari na kuwapatia tarakilishi, laptops na mitandao ya interneti, na vifaa vyote vya logisti ikiwa ni pamoja na printa za kisasa, makini za kupiga chapa na skrini zilizo na shughuli za kuonyesha, pamoja na kutoa vitengo visivyo na waya vilivyosambazwa juu ya kumbi nne zilizo na wifi ,pamoja na vifaa vya Wi-Fi kutoa huduma za mtandao kupitia mitandao 4G, na pia kuandaa huduma za mawasiliano ya tovuti, mtandao na kuonyesha skrini kwenye ukumbi uliotengwa kwa sherehe ya kupiga ngoma ya ubingwa mnamo Septemba ijayo, mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mhandisi Raafat Hindi, Naibu wa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Miundombinu.
Comments