Ahmed Ahmed anatangaza kuundwa kwa kamati ya usalama ili kuepuka ghasia katika Kombe la Afrika 2019.

Ahmed Ahmed, "Rais wa Shirikisho la Soka la kiafrika (KAF)", ametangaza makubaliano pamoja na  serikali ya kimisri kuunda kamati ya usalama ili kukabiliana na ghasia au ugaidi ambazo huenda hutokea wakati wa  Kombe la Mataifa ya Afrika2019,

Ahmed Ahmed alisema kauli yake wakati wa ziara yake kwa Afrika Kusini "Hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuhakikisha kwamba hakuna kitu kitatokea wakati wa kukaribisha kwa michuano, duniani mwote. Usalama ni tatizo la kimataifa na si  la kimisri tu",

Aliongeza "Ndiyo, ni bahati mbaya kwamba hatuwezi kuthibitisha kwamba hakuna kitu kitatokea wakati wa michuano yoyote, lakini tumekubaliana na serikali ya kimisri kuunda kamati ya usalama ili kudhamini kwamba hakuna kitu chochote kitatokea na kukabiliana na matukio yoyote ambayo yanaweza kutokea wakati wa Kombe la Afrika. 

Comments