Huenda 2021 inaweza kuwa mwaka wa mpira wa mikono nchini Misri
Mohamed Sanad, Mrengo wa timu ya kitaifa ya Misri na klabu ya Nimes ya Ufaransa, anaamini kuwa timu yake ndio timu ya ndoto sasa hivi, na 2021 inaweza kuwa mwaka wa mpira wa mikono huko Misri.
Misri yapokea michuano ya dunia kwa wachezaji wa kiume wa mpira wa mikono mnamo Januari, pia itashiriki katika Michezo ya Olimpiki huko Tokyo msimu wa joto ujao.
Mohamed Sanad hakuanza na mpira wa mikono, lakini alishughulika kati ya viwanja vya Boga na mpira wa kikapo ili kupata mchezo wake mpendwa.
Mnamo 2001, wakati alikuwa na umri wa miaka 10, alishuhudia kufanikiwa kwa timu ya mpira wa mikono ya Misri na kufanikiwa nafasi ya nne kwenye michuano ya dunia kama timu ya kwanza isiyo ya Ulaya kufikia mraba wa dhahabu.
Michuano hiyo ilikuwa sababu ya Mohamed Sanad kubadili mwelekeo kwa mpira wa mikono hadi anakuwa moja ya nguzo kuu ndani ya timu.
Muhammad Sanad anaona kwamba timu ya nchi yake ya kisasa ina uwezo wa kufikia majukwaa ya michuano ya dunia na Olimpiki ya Tokyo.
Sanad alisema katika mazungumzo na tovuti Olympic Channel "Nina ndoto ya kuhakikisha michuano miwili ya kihistoria na Misri mnamo 2021".
Aliongeza, "Ndoto yangu ni kushinda medali ya Olimpiki na nyingine kwenye Michuano ya Dunia, tunaweza kuihakikisha, basi Kiwango cha timu ni nzuri na tuna kocha mkubwa".
Sanad akendelea "Tunaweza kuipata timu ya ndoto ya Misri kwa kushinda medali, halafu tunaweza kusema kuwa sisi ni timu ya ndoto sasa".
kuhusu siri ya ustadi wa Misri katika mpira wa mikono mnamo kipindi cha hivi karibuni, Sanad alielezea, "kwa sababu ya mabadiliko ya mawazo ya wachezaji. Zamani, wakati tulipocheza dhidi ya Ufaransa, kwa kweli tulishindwa kwa pointi 10".
Sanad alisema, "Kufikiria na mawazo hayo husababisha huzuni na hautakufikisha kile unachotaka kufikia".
Alisisitiza "Lakini sasa unaona wote wanaamini katika uwezo wako na timu inaweza kushinda, na tunaenda huko na tunafanya hivyo".
Na nyota wa Timu ya kimisri alieleza kuwa "Hakika timu za Ulaya ndizo bora zaidi ulimwenguni na zina nguvu sana na sio rahisi kuzishinda, lakini tunaweza kufanya hivyo".
Akaendelea, "Hiyo ndiyo tunayoijenga na kujaribu kuthibitisha kwa ulimwengu kuwa tunakuja, tunakuja kufanya kitu kikubwa".
Timu ya chini ya miaka 19 ya Misri ilifanikiwa kuhakikisha michuano ya dunia mwaka uliyopita kama timu ya kwanza isiyo ya Ulaya kufanya hivyo.
Sanad alisema, "Tunaunda kizazi chenye nguvu sana. Mchanganyiko baina ya uzuri wa vizazi hufanya mpira wa mikono huko Misri uwe mzuri wakati ujao".
Sanad alifunua, "Msimu ujao utakuwa moja ya misimu mikubwa katika safari yangu, kucheza michuano ya dunia nchini mwangu na kufikia Michezo ya Olimpiki".
Alimaliza mazungumzo yake, "Natumai kutoshinda chini ya medali katika michuano hiyo miwili. Mwaka wa 2021 unaweza kuwa mwaka wa mpira wa mikono wa Misri".
Comments