Sobhy ahudhuria mkutano wa Kamishna ya Umoja wa Afrika pamoja na mawaziri waafrika wa michezo

Jumanne, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo ya kimisri , alishuhudia mkutano wa Umoja wa Afrika pamoja na mawaziri wa michezo katika nchi wanachama, kwa ajili ya kujadili njia bora katika uwanja wa michezo ili kukabiliana na janga la Corona,  kwa ushiriki wa Waziri Sayed Ali Khaled, Waziri wa vijana na michezo na mkuu wa ofisi ya kiutendaji ya baraza la mawaziri  waafrika wa vijana na michezo , na Bi. Amira El_Fadel, Mwenyekiti wa Kamishna ya Afrika ya masuala ya jamii, na mawaziri waafrika kadhaa. 


Mkutano huo ulihusisha jukumu ambalo nchi huchukua kukabiliana na virusi vya Corona, pamoja na mipango ya siku za usoni na jinsi ya kukabiliana na virusi. 


Katika hotuba yake, Dokta Ashraf Sobhy alithibitisha kwamba Wizara ya Vijana na Michezo inaratibu kila wakati na Kamati ya Matibabu na Kamati Kuu ya kukabiliana na Corona na hatari ya virusi hivi, akiongeza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo imetoa kadi kadhaa za kurudi kwa shughuli za michezo katika michezo mbalimbali kwa kushirikana na Kamati ya Olimpiki ya Misri na Kamati ya Matibabu, akisisitiza umuhimu wa umbali wa kijamii , kuchukua hatua zote za Kinga zilizofuatwa na ukaguzi wa mara kwa mara na wa kudumu kwa vifaa vya vijana na michezo katika kuchukua hatua zote muhimu za kupunguza virusi. 

Comments