Waziri wa vijana na michezo akutana na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DHL watafute njia za ushirikiano kati yao

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo, leo amekutana  na Bwana Sour Soliman Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DHL huko Mashariki ya kati na Afrika kaskazini , na Bwana Ahmed El Fangary mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DHL huko Misri ili kutafuta njia za ushirikiano kati ya Wizara na kampuni mnamo awamu ijayo . 


Sobhy alielezea furaha yake kwa kukutana na maafisa wa kampuni ya DHL , wakati ambapo itakakuwepo ushirikiano kati ya pande hizo mbili  mnamo awamu ijayo katika miradi mbalimbali na mipango iliyofanywa na Wizara , na utaratibu utawekwa ili kushirikiana pamoja katika shughuli kadhaa za kufikia idadi kubwa zaidi ya vijana katika Jamuhuri . 


Akiongeza kuwa mpango wa Wizara mnamo awamu ya kisasa ni kupanuka katika shughuli na mafanikio yanayofanyika kwa ajili ya kufikia idadi kubwa zaidi ya vijana  na kuhakikisha faida kubwa kwa watu wengi wa jamii .

Comments