Waziri wa Michezo na Gavana wa Port Said wakishuhudia mazoezi ya wachezaji wa Skwashi miongoni mwa Mradi wa Kitaifa kwa talanta katika mji wa michezo

Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, akiambatana na Meja Jenerali Adel Ghadhban, Gavana wa Port Said, jioni ya Alhamisi, walishuhudia mafunzo ya wachezaji wa Skwashi walioshiriki katika Mradi wa Kitaifa  kwa talanta na  Bingwa wa Olimpiki unaotekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo.


Mji wa michezo mkoani Port Said  unakaribisha mafunzo kwa wachezaji katika kikosi cha Skwashi mbele ya makocha na mafundi maalum na viongozi kadhaa wa Wizara hiyo, kwa kuzingatia kuanza tena kwa mafunzo ya Mradi wa Kitaifa kwa talanta na bingwa wa Olimpiki, ambao ni pamoja na Taekwondo, Judo, kuinua uzito , Mieleka , mpira wa mikono , mpira wa kikapu , Skwashi , michezo za nguvu , Dilaha, Tenisi ya meza. "


Waziri wa Vijana na Michezo alisifu kiwango cha kipekee cha wachezaji wachipukizi wa Skwashi walioshiriki katika mradi huo, waliochaguliwa kulingana na misingi ya kisayansi, akiashiria kujali kwa Wizara hiyo kwa Skwashi kwa kushirikiana na Shirikisho la Misri kwa Mchezo huo, kutoa msaada kamili kwa wachezaji, na kufunua na kudhamini vipaji ili kudumisha mwongozo wa Misri katika mchezo huo kwa kiwango hicho duniani.


Wizara ya Vijana na Michezo ilizindua vipimo vya uteuzi kwa Mradi wa Kitaifa kwa wenye talanta  wa Skwashi chini ya uangalifu ya Benki ya Al-ahly kama sehemu ya Mradi wa Kitaifa kwa talanta na Bingwa wa Olimpiki Januari iliyopita ili kuchagua wanariadha bora 250 na wachezaji kutoka kwa waliochukua majaribio katika mikoa ya Kairo na Port Said, na waombaji walijaribiwa na kuchaguliwa na wataalamu wa juu katika uwanja wa Skwashi kwa kushirikiana na Shirikisho la Skwashi la Kimisri, wana wa mashahidi wa majeshi, polisi na mayatima wanawakilisha 20% ya washiriki, kama dalili kwamba serikali ya Misri haisahau wana wake waliotoa maisha yao kwa ajili ya nchi hiyo.


Wavulana wanashiriki katika mradi huo ambao walizaliwa mnamo 2012, 2013 na 2014 katika mchezo wa Skwashi . Kuunda Sehemu kubwa kwa wachezaji wa Skwashi , na kuandaa vizazi wapya kwa mchezo.


Waziri wa Vijana na Michezo na Gavana wa Port Said pia walifanya ziara ya ukaguzi ndani ya Jiji la Michezo, ambayo ni pamoja na bwawa la kuogelea la Olimpiki, viwanja vingi, viwnja vya tenisi ya ardhi , na uwanja wa mpira wa miguu, na vyuo vikuu vya michezo vilivyoanzishwa katika jiji hilo vilifuatiliwa baada ya kuanza tena kwa shughuli kwa mujibu wa udhibiti na hatua za tahadhari kuchukuliwa ili kukinga na virusi vipya vya Corona .


Kwa upande wake, Gavana wa Port Said alielezea kuwa mji wa michezo wa serikali ni moja wapo ya majengo ya michezo ambayo hushuhudia mipango mingi ya michezo na miradi na shughuli za vijana kwa mwaka mzima, akisifu ushirikiano mzuri na Wizara ya Vijana na Michezo katika kutekeleza mipango ya wana wa Port Said na kuboresha miundombinu ya michezo mkoani .


Comments