Waziri wa Michezo aongoza mbio za Baiskeli huko eneo jipya la Handaki za Port Said

Asubuhi, Ijumaa, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, akiambatana na Meja Jenerali Adel Ghadhban, Gavana wa Port Said, ameongoza mbio za Baiskeli, pamoja na ushiriki wa kikundi cha vijana na wasichana, na mahudhurio ya viongozi kadhaa wa wizara hiyo.

 Mashindano ya Mbio yameanza na umbali wa km 8 huko eneo la Handaki za Port Said.


Waziri wa Vijana na Michezo ameusifu mradi wa Handaki za Port Said, unaozingatiwa kama mmoja wa miradi ya maendeleo ya kitaifa inayofanyika nchini chini ya uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, anayeongoza Mwelekeo wa maendeleo ya nchi hiyo katika sekta tofauti, akiashiria mafanikio ya wizara hiyo  katika utekelezaji wa matukio kadhaa katika miradi ile kwa lengo la kuwapasha vijana kwa kile kinachotokea kweli kama miradi mikubwa na kutumia vizuri thamani ya michezo katika kutupa jicho kwa miji, na miradi mipya.


Dokta Ashraf Sobhy aliashiria shime ya Wizara ya kueneza utamaduni wa mazoezi ya michezo ndani ya jamii kati ya vijana na raia, na kuifanya michezo kuwa njia ya maisha kama utekelezaji wa mhimili mmoja mkuu wa mkakati wa Wizara kupitia Matukio, Mbio na Shughuli za michezo zinazotekelezwa mara kwa mara katika mikoa yote ya Jamhuri, akiashiria umuhimu wa michezo katika maisha ya mtu binafsi, na mchango wake wa kumkua kwa njia nzuri.


Waziri wa Vijana na Michezo aliashiria mpango wa "Baiskeli yako ... Afya yako" unaotekelezwa na Wizara kama kutoa Baiskeli kwa vijana na raia  ili kununua kwa bei nafuu, na hadi sasa awamu mbili zimetekelezwa kwake, na huendelea sasa kuzindua awamu mpya inayojumuisha idadi kubwa ya Baiskeli zinazofaa mahitaji ya vijana, akieleza Uangalifu wa Rais wa mpango huo ni Dalili ya nia wazi ya utunzaji wake wa kueneza mazoezi katika jamii, ambapo michezo inachangia kuboresha hali ya mwili na afya kwa watumiaji wake na ni njia rahisi ya usafiri.


Waziri ameongeza kuwa mhimili wa maendeleo ya michezo ni mmoja wa mihimili mikuu inayotumika vyema kutokana na Wizara katika kuendeleza sekta ya michezo, pamoja na kukuza Ajenda ya maendeleo ya michezo ili ijumuishe matabaka yote ya jamii, na kutekeleza mipango ya kuboresha mtindo wa afya wa raia kupitia mazoezi ya michezo.

Comments