Mayar Sherif ashinda mchezaji wa Czech katika mashindano wazi ya Prague ya Tenisi

Bingwa Mmisri Mayar Sharif, mchezaji wa Tenisi, na aliyefikia Olimpiki ya Tokyo, alifanikiwa kushinda mechi yake ya kwanza kwenye Mashindano wazi ya Prague ya Tenisi  huko Jamhuri ya Czech, dhidi ya mchezaji wa Czech Linda Nsokova kwa vikundi viwili safi, matokeo yao yalikuwa kama ifuatavyo: 7/6, 5/7.

 

 Huu ni ushiriki wa pili wa Mayar Sharif mnamo mwaka huu kwenye michuano wazi ya Prague, ambapo alishiriki katika mashindano yenyewe mnamo Julai iliyopita.

 

Mashindano wazi ya Pargue yanachukuliwa kuwa mashindano "Challenger" na ni mashindano muhimu katika Tenisi ya wanawake.


Mayar Sherif anatafutia kushinda ubingwa zaidi mnamo kipindi kijacho kimataifa ili kuendeleza katika uainishaji wa mchezo huo ulimwenguni, hasa kwani anayo rasilimali kubwa za kiufundi zinazomsaidia kushinda mashindano zaidi na zaidi na kufikia fainali.

 

 Mayar Sherif alikuwa ameshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Tenisi ya ardhi kwenye kikao cha Michezo ya Kiafrika huko Morocco, na Mayar Sherif alifanikiwa kushinda katika mechi ya fainali ya wanawake moja dhidi ya Storm Simmons ambaye ni mchezaji wa Afrika Kusini na kufanikiwa kushinda 2-0.

 

Mayar Sherif alifikia kikao cha michezo ya Olimpiki huko Tokyo, kulingana na matokeo hayo, na Mayar Sherif ndiye mwanariadha wa kwanza wa Misri anayefikia Olimpiki kwenye historia ya mchezo huo.


Comments