Mayar Sherif, Bingwa wa Misri katika michezo ya Tenisi, na aliyefikia michezo ya Olimpiki ya Tokyo, aliweza kushinda katika mechi yake ya pili katika mashindano wazi ya Prague huko Czech, dhidi ya mchezaji wa Hungary "Delma Galfy "kwa vikundi viwili mbele ya kikundi kimoja, kwa tija : 7/6 - 6/1 - 6/3.
Na inatarajiwa kuwa Mayar Sherif, Bingwa wa Misri katika Tenisi atacheza dhidi ya mchezaji wa Serbia "Evana Urovitch" katika duru ya 16 ya mashindano hayo kesho Jumanne.
Ushiriki huo unazingatiwa wa pili kwa Mayar Sherif mnamo mwaka huu katika mashindano wazi ya Tenisi, ambapo alishiriki mnamo Julai iliyopita katika mashindano yenyewe.
Mashindano wazi ya Prague yanazingatiwa miongoni mwa uainishaji wa ( Challenger ) na hayo ni miongoni mwa mashindano muhimu katika Tenisi ya wanawake.
Mayar Sherif anatafutia kushinda michuano zaidi mnamo kipindi kijacho kimataifa kwa ajili ya kuchukua nafasi bora zaidi katika uainishaji wa kimataifa, hasa, anayo rasilimali kubwa za kiufundi zinazomsaidia kushinda medali zaidi na zaidi na kufikia fainali.
Mayar Sherif alikuwa ameshinda medali ya kidhahabu ya mashindano ya tenisi ya ardhi kwenye kikao cha michezo ya Kiafrika yaliyofanyika nchini Morocco, na aliweza kushinda katika mechi ya fainali kwa wanawake dhidi ya Storm Simmons ambaye ni mchezaji wa Afrika Kusini na kufanikiwa kushinda kwa 2-0.
Mayar Sherif alifikia kikao cha michezo ya Olimpiki ya Tokyo, kulingana na matokeo hayo, pia Mayar Sherif ni mchezaji mmisri wa kwanza aliyefikia michezo ya Olimpiki katika historia ya michezo huo.
Comments